1. Amri na hukumu katika maandiko ya Qur-an na Biblia
Jamii ya imani zote yaani Ukristo na ile ya Uislam, zinatambua kuwepo kwa Manabii na Mitume ambao Mungu aliwapa maono na mafunuo ya aina
mbalimbali ili kuwasaidia waja wa mungu.
Miongoni mwa manabii hao mmoja wapo ni Nabii Musa (alayhi salaam) ambaye katika imani ya Kiislam hutambuliwa kama Nabii aliyeongea na Mungu (Takalama llahu)
Mafunuo ya Qur-an yakiungana na yale ya awali ya Biblia huweka wazi mahali na jinsi nabii huyo alivyopata utume [unabii wake, katika kitabu cha Biblia habari hizo hupatikana katika kitabu cha Kutoka sura 3:1-10,
Maandiko hayo huungwa mkono na yale ya kitabu cha Qur-an tunaposoma
katika kitabu hicho katika sura ifuatayo:-
Surat Taha 20:3 "Nami nimekuchagua (kuwa mtume) basi yasikilize
unayoletewa (yanayofunuliwa kwako) wahyi."
Hapa Qur-an huonyesha tukio la kusimikwa kwa Nabii Musa na kupewa agizo la utame kwenda kwa Farao, [Firauni], hivyo hii inathibitisha vile ambavyo vitabu vyote hukubaliana juu ya utume wa nabii huyu [Musa alayh salaam],
Katika harakati za utume huo wa Nabii Musa ndipo tunaona akiwa katika safari ngumu ya kuwakomboa wana wa Israeli, na hatimaye baada ya kuvuka milima na mabonde anawafikisha chini ya Kilima kiitwacho Sinai.
Kama tujuavyo kibiblia kuwa hapo ndipo Musa alipo kabidhiwa mbao mbili za sheria na hukumu za Mwenyezi Mungu, ndivyo vivyo hivyo Qur-an pia huelezea kama tunavyo soma katika sura hii.
Qur-an Surat Al- A’raf 7:144-145
Akasema (Mwenyezi Mungu) "Ewe Musa mimi nimekuchagua juu ya watu wote kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu Basi pokea haya “niliyokupa" na uwe miongoni mwa wanaoshukuru.
[145] - Na tukamwandikia katiha mbao kila kitu mawudha (ya kila namna) na maelezo ya kila jamho "Basi yashike kwa imara bora haya, Karibu nitakuonyesheni miji ya wavunjao amri zetu ilivyoharibika na nitakuwalisheni ninyi.
Ndugu msomaji wangu. kama umefuatilia kwa uzuri aya hizo, yako mambo kadhaa ambayo utakuwa umeyagundua, binafsi nimeng'amua mambo yafuatayo:-
1.Kuna vitu ambavyo Musa aliitwa na kukabidhiwa na Mungu mwenyewe
(aya ya 144).
2. Vitu hivyo ni amri za Mungu, na aliye vikabidhi kwa Musa ni Mungu
Mwenyewe.
3. Aliye ziandika Amri hizo ni Mungu yeye mwenyewe (na tukamuandikia -
rejea aya ya 145)
4. Mungu hakuhitaji watu wazivunje amri hizo, ball wazishike kwa uhimara.
5. Mungu hakuwa na msamaha kwa wanao vunja amri zake tangu zamani.
Mpendwa msomaji kwa misingi hiyo, basi tunaona maandiko ya kitabu hiki cha msahafu wa Qur-an yanakubali tena kwa uwazi tu juu ya kuwapo kwa Amri za Mungu tena amri hizo hazikupaswa kuvunjwa, swali linalobakia ni kuwa, Amri hizo ni zipi? Naje Qur-an huzitaja amri hizo?
Katika utafiti wangu unaotokana na kusoma Qur-an mara kwa mara, nimeweza kugundua vile ambavyo Qur-an nayo hufunua amri hizo kumi ingawa si kwa maneno yanayo wiana sawa na yale ya Biblia bali wazo hubaki pale pale, kwa jinsi hiyo basi ninao ujasiri wa kueleza wazi kuwa Qur-an nayo huzitaja amri zote kumi kama ilivyo tangulia kukiri kuwa Mungu alikabidhi amri hizo kwa Nabii Musa, na yeye mwenyewe ndiye aliyeziandika, hebu na tuone maarifa hayo mapya ndani ya Qur-an katika ulinganifu na yale ya awali ya Kibiblia.
Amri na hukumu katika Qur-an na Biblia.
Biblia Qur-an
- Kutoka 20:1-3 usiwe na miungu Mingine - Qur-an 17:22 usifanye miungu mingine
- Kutoka 20:4 usijifanyie sanamu ya kuchonga - Qur-an 26:68-73 Je hizo sanamu
zitawasikia
- Kutoka 20:7 usilitaje bure jina la Bwana - Qur-an 7:180 usiharibu utukufu
Mungu wako wa majina ya mungu wako.
- Kutoka 20:8 ikumbuke siku ya Sabato iutakase - Qur-an 7:54 hakika mola wenu
siku sita fanya kaziya saba ni sabato ya mwenyezi mungu aliumba mbingu na
Bwana Mungu wako. ardhi kwa siku sita kasha
akastarehe[siku ya saba]
- Kutoka 20:12 waheshimu baba yako - Qur-an 17:23 tuwaheshimu watu walio songa
na mama yako [kuzidi] umri.
- Kutoka 20:13 usiue - Qur-an 4:29 msijiue wala msiue wenzenu
- Kutoka 20:14 usizini - Qur-an 17:32 wala msiikaribie zinaa
-Kutoka 20:15 Usiibe - Qur-an 17:35 pimeni kwa mizani iliyo sawa
- Kutoka 20:16 usimshuhudie jirani - Qur-an 22:30 mjiepushe na
yako uongo usemi wa uongo
- Kutoka 20:17 usitamam mali ya mtu mwingne - Qur-an 17:34 msitamani mali ya
yatima.
Hivvo ndivyo tuonavyo Qur-an ikizitaja amr hizo katika aya tofauti na mfumo tofauti. kwa hiyo kwa msingi huo tunaweza sasa kufuatilia vyema mada yetu hii ihusuyo siku ya ibada ya Sabato katika mafunuo ya Qur-an.
Jambo Kuu
Kupitia uchambuzi huu wa amri kumi za Mungu- tumeweza kuona Qur-an ikiitaja siku ya saba yajuma na ya kuwa siku hiyo Mungu hakufanya kazi yeyote zaidi tu ya kustarehe- na hivyo Mungu alimjulisha Musa ill awahusie watu wake juu ya Jambo hili kama amri ya kuitambua siku hiyo. Ya mapumziko na kustarehe ambayo bila shaka ndiyo inayoitwa Sabato.
Ninaamini ndugu msomaji tumekwenda sambamba katika uchambuzi huu wa
mwanzo utakao tupa mwanga mkubwa wa kuelewa vyema maarifa haya juu ya
siku ya Ibada ya kweli, pamoja na hayo ninaamini kuwa huenda ukasumbuliwa sana hasa unaposikia neno Sabato- hivyo ili kukuandaa vyema ni vyema nikakupatia maana ya neno hili Sabato, nikihusisha na lugha mbali mbali za kigeni katika matamshi ya neno hili.