Wahasisi Wetu
Mwinjilisti
Godfrey J. Machota
Mwinjilisti
Osward G. Dorogwe
Historia yetu
Tazama Uzinduzi wa Ministry
Njozi ya huduma kwa njia media/mtandao ilianza mwaka 2010 wakati tukiwa kidato cha tano Ndanda sekondari, tulianza kwa kujiita waberoya, nakumbuka tulikuwa tunarekodi mahubiri ya audio kwa kutumia simu.
Tukiwa sekondari kwa kushirikiana na ASSA tulifanikiwa kufanya mikutano miwili na kwa mara ya kwanza tulihubiri kwa njia ya projecta kwa kutumia slides jambo ambalo lilisisimua watu sana.
​
Baada ya kumaliza sekondari tuliamua kubadili jina na kuanza kuiita huduma yetu Three Angels Ministry ambayo kwa sasa inamiliki Habari njema Online TV na Radio, tumekusudia kuipeleka injili ya malaika watatu mbele kwa neema ya Yesu ili kuwaandaa watu kwa ajili ya marejeo ya mara ya pili ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo
​
Huduma ya Three Angels Ministry ilizinduliwa rasmi mwaka 2014 na Mchungaji Richard G. Kaniki aliyekuwa katibu mkuu wa jimbo la Southern Highland Conference (SHC) tukiwa katika Chuo kikuu cha sayansi na tekinologia Mbeya (MUST)