top of page

MAHALI ILIPO JEHANUM

hell-on-earth-large.jpg

       Biblia inasema waziwazi kwa uthabiti kwamba moto huo unawala hao waovu papa hapa “juu ya upana wa nchi.”  Kila mwandishi wa Biblia anayezungumza juu ya somo hili la jehanum anaongeza maarifa mapya juu ya hiyo mauti ya pili ya wale waovu.  Petro anaeleza hivi:  “Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya  kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.”  2 Petro 3:7.  Kisha anaendelea kueleza habari ya ile siku ya Bwana itakayoviyeyusha viumbe vya asili kwa moto mkali sana. 

 

        Lugha ya Petro iko wazi sana kuhusu mahali pa adhabu kwa wale wasiomcha Mungu. Anasema kwamba nchi hii imewekwa akiba kwa moto ule utakaoleta hukumu na maangamizi kwa waovu.   Adhabu yao itakuwa katika nchi [dunia] hii.  Isaya alitangaza hivi,  “Maana ni siku ya kisasi cha BWANA, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.  Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na ardhi yake itakuwa lami iwakayo.”  Isaya 34:8,9. 


     Nabii huyo anaonyesha picha ya sayari hii nzima ikifunikwa na moto ulao.  Hata vijito na mavumbi vinageuzwa na kuwa lami inayolipuka na kuwaka moto mkali na kiberiti.  Isaya anasema kwamba hicho ndicho kisasi chake Mungu na “thawabu” yake wakati wa mwisho wa pambano hilo. 

Daudi anaongezea juu ya ushuhuda huo kwa maneno haya,  “Awanyeshee wasio haki mitego, moto na kiberiti na upepo wa hari, na viwe [vitakuwa – KJV] fungu la kikombe chao.”  Zaburi 11:6.   Zingatia kwamba anatumia karibu maneno yale yale kama Yohana na Petro katika kuelezea ajali itakayowapata waovu.  Wote wanakubaliana kuhusu mahali pa adhabu hiyo (kuwa ni nchi [dunia] hii)  na njia iliyochaguliwa kwa adhabu hiyo (moto).


     Jambo hilo hutuleta kwenye ukweli mkuu wa tatu kuhusu somo hili la jehanum.  JEHANUM KAMA MAHALI PA ADHABU ITAKUWA NI DUNIA HII AMBAYO ITAGEUZWA NA KUWA  ZIWA LA MOTO KATIKA SIKU ILE YA HUKUMU.  Lakini jambo hili pia huzusha maswali fulani ya kuvutia sana kuhusu ajali itakayowapata wale watakaopotea.  Mojawapo ya maswali hayo  yanayowachanganya sana watu na kuwaletea utata mwingi sana linahusu muda utakaotumika kwa adhabu hiyo.  Je, ni kwa muda mrefu jinsi gani waovu wataendelea kuwa hai na kuteswa katika moto ule? 


     Hakuna awezaye kujibu swali hilo kwa usahihi kabisa kwa sababu Biblia inasema kwamba wataadhibiwa kulingana na kazi zao [matendo yao].  Hii humaanisha kwamba patakuwa na viwango  vya adhabu.  Wengine watateswa kwa muda mrefu kuliko wengine.  Lakini jambo moja tuwezalo kusema kwa hakika kabisa ni hili  -  waovu hatawaendelea kuishi katika moto ule milele na milele.
 

bottom of page