Je Bwana Yesu Alikuwa Muislamu?
Ndugu mpendwa tutakubaliana kuwa katika Ulimwengu huu wenye msongamano wa imani tofauti na nyingi.kuna maswali mengi juu ya imani hizo kwa kadri ya mafunuo ya vitabu vyake. Jamii ya watu wanao fuata imani ya Uislam wamekuwa na maswali mengi dhidi ya imani ya kikristo hivyo mimi msaidizi wako katika kazi ya uinjilisti kwa waislam,nimeona vyema kujitafutia usahihi wa mambo hayo na hivyo kukuandikia makala hii ndugu msomaji wangu ili uweze kujivunia maarifa haya muhimu.
Hoja zinazojengwa kuhusiana na mada hii:
Inaonekana katika kitabu cha Injili ya Luka 4:16 Yesu aingia katika Sinagogi ana tafsiri yaonyesha sinagogi ni Msikiti. Je Yesu alikuwa na Imani ya Kiislam maana Misikiti ni ya Waislam.
Mpendwa ninaomba ufuatilie kwa makini ikiwa unajali usalama wa roho za wengine wanao potea katika mambo yahusuyo imani maana ni hakika kuwa watu wengi wamepotoshwa kwa maswali haya na hivyo imani zao kutindikiwa. Hivyo ninaomba tuanze kufanya uchunguzi wa kina wa maswali hayo.
YESU AINGIA KATIKA SINAGOGI JE ALIKUWA NI MUISLAM? MAANA SINAGOGI NI MSIKITI.
Kigezo cha sinagogi kimekuwa ni kelele kubwa kwa watu na jamii ya kiislam na lengo lao kubwa ni kutaka kumfanya Bw. Yesu aonekane kuwa sinagogi ni msikiti.
HEBU TUCHUNGUZE KWA KINA NENO HILI
Sinagogi au Masinagogi chimbuko lake ni baada ya ya wana wa Israel kwenda katika uhamisho wa Babeli na walipo rudi mnamo mwaka 587 walikuta hekalu lao lime vunjwa pale Yerusalemu hivyo chini ya uongozi wa Nabii Ezra waliamua kujenga vijijengo vidogo kwaajili ya shughuli za ibada na kutafakari Torati ya Musa, majengo hayo na mikutaniko hiyo kwa asili ndio iliyopewa jina na kuitwa “Masinagogi” wakati wa kipindi cha Agano jipya jina hilo kiasili lilimaanisha:- “kukutanika” au “kikutanisho”. THE BOOK , DONFLEMING UK 561.
Swali:
Mbona Biblia inasema kuwa Sinagogi ni Msikiti wa Wayahudi?
UFAHAMU;
Katika tafsiri ya Biblia Union Version yapo maneno kadha wa kadha yenye asili ya lugha ya Kiarabu na Kiswahili cha kimvita hii ina tokana na mfasili(Mmisionary) wa kwanza aliye tafsiri biblia kumshirikisha mzee (Shekhe) ili aweze kusaidiana naye katika kazi hiyo iliyo onekana kuwa ngumu kwake kutokana na kutojua vizuri Kiswahili hivyo ndiyo maana utakuta maneno mengi yenye asili ya Kiarabu ndani ya Biblia (Tazama Mifano).
-
kumbukumbu 16:16 Neno (IDI) limewekwa.
-
Yuda 1:4 Neno (Makafiri) pia.
-
1 Samweli 5:8 Neno (Mashekhe) limewekwa.
Pamoja na hayo alipo tafsiri neno hili Sinagogi kuwa ni msikiti haku tafsiri kwa kuzingatia utalaamu wa lugha bali alifananisha mambo Fulani Fulani yanayo tendeka katika majengo hayo mawili yaani Sinagogi na Msikiti na ndipo akafasiri kuwa Sinagogi ni Msikiti wa Wayahudi kwa kulinganisha baadhi ya matendo yanayo fanana baina ya majengo hayo mawili.
Aina ya tafsiri iliyotumika kitaaluma;
Kwa kadri ya taaluma ya Kiutafsiri mtafsiri huyo wa Biblia ametumia moja kati ya aina kuu mbili za kiutafsiri ambapo aina ya kwanza ni ile ya tafsiri “Shabihifu” na ya pili ni tafsiri “Maanifu”.
Hivyo kimsingi katika kutoa maana hiyo ya Sinagogi- Msikiti wa Wayahudi. msaidizi huyu katika utafsiri wa Biblia alionekana kukosa namna ya kulieleza neno hilo sinagogi na ndipo akaadhimu kutoa tafsiri hiyo ambayo kitaaluma siyo tafsiri “Maanifu” (haiendani na asili ya neno katika lugha husika) bali alitumia tafsiri “Shabihifu” inayozingatia mambo machache yanayofanana baina ya vitu viwili ndiyo maana alisema ni Msikiti wa Wayahudi hivyo kamwe hakusema kuwa ni Msikiti wa Waislam maana alitambua kuwa katika wakati huo bado uislam haukuwa umeanzishwa.
HEBU SASA TUANGALIE MAANA NA MAJINA YA MAJENGO YA IBADA ILI TUONE UKWELI WA NENO HILI SINAGOGI KATIKA UTAALAMU WA WA LUGHA
Je Sinagogi laweza kuwa ni Msikiti katika uasili wa lugha?
Qur-an Surat 22:40
Andiko hili linataja majina ya majengo mbalimbali ya ibada ikiwemo na sinagogi ingawa halikuwekwa kwenye tafsiri ya Qur-an ya Kiswahili ila tutalichunguza kwa watafsiri wengine wa Qur-an hususani tafsiri ya kingereza iliyotolewa na Mwanazuoni wa Kislam ndugu Yusufu Ally.
Qur-an ya sura ya 22 :40 katika tafsiri ya kiingereza inaeleza yafuatayo:-
Those who have been expelled from their homes unjustly but only because they say our Lord is Allahfor had it not been that Allah checks one by means of another have been pulled down Monasteries Churches Sinagogues and Mosques …….
Tafsiri ya aya hiyo katika Kiswahili,
Ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki ila kwasababu wanasema mola wetu ni Mwenyezi Mungu, na kama Mwenyezi Mungu asingeliwakinga watu baadhi yao kwa wengine bila shaka yangelivunjwa Mahekalu, Makanisa, Masinagogi na Misikiti………….
Katika sehemu hii tafsiri hiyo ya Qur-an iliyotolewa kwa lugha ya kingereza inataja wazi kuwepo kwa majengo mawili kati ya manne ambayo kwahakika ndiyo yanayosumbua watu wengi hata hivyo Qur-an inaonekana tena kwa uwazi ikiyatofautisha majengo hayo ambayo ni Masinagogi na Misikiti. Hilo linaonekana siyo tu katika tafsiri bali hata katika maandishi ya lugha ya Kiarabu.
Fuatilia majina ya majengo hayo katika matamshi ya kiarabu na maana zake hapo chini.
BILASHAKA YANGELIVUNJWA
KISWAHILI KIARABU
1) Mahekalu Swawamiyu
2) Makanisa Wabiyauni
3) Masinagogi Waswalawatun
4) Misikiti Wamasaajidu
Katika ushahidi huu yametajwa majengo manne lakini mwishoni tunakuta majengo mawili na jengo la kwanza linaitwa “Swalawatuni” yaani Sinagogi na la pili “Masjid” yaani “Msikiti” hivyo haya ni majengo yaliyotofauti kabisa maana sinagogi ingekuwa ni msikiti lisinge itwa Swalawatuni kwa kiarabu bali lingeitwa Masjid hivyo hii inadhihilisha kuwa katika maana halisi ya lugha sinagogi kamwe haliwezi kuwa ni msikiti hivyo ni kama nilivyoeleza mwanzo kuwa neno sinagogi lilimaanisha kikutanisho au kukutanika.
KIGEZO CHA YESU KUINGIA KATIKA SINAGOGI SIYO KIGEZO SAHIHI CHA KUFUNDISHA KUWA YESU NI MUISLAM.
Hebu fuatilia fungu hili la Biblia;
MATENDO YA MITUME 17:1
Akiisha kupita kati ya amfipoli na Aporonia akafika Thesalonike ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi na Paulo akaingia mle walimo akahojiana nao kwa maandiko sabato tatu.
Endapo umefuatilia fungu hilo kwa makini unaweza kujiuliza swali lifuatalo ………….
Ikiwa kuingia tu kwenye sinagogi kulimaaninsha kuwa mtu huyo Yesu ni Muislam je Paulo naye kwa tendo hilo lakuingia humo alikuwa Muislam?
Jambo la kushangaza hata wale wanaotoa fundisho hili humkataa Paulo kwa kadri ya imani yao na huku wakijivisha kitanzi kwa madai hayo kuwa mtu huwa muislam kwa kuingia katika Sinagogi. (Alichofanya Yesu katika Sinagogi hakiwiani na Misikiti ya Waislam.)
Luka 4:16 – 17 Yesu apewa chuo cha nabii Isaya, je Waislam leo hii wanachuo cha nabii Isaya Msikitini? (La Hasha ) hii inaonyesha utofauti mkubwa uliopo baina ya Masinagogi na Msikiti ingawa ni vitu vichache tu vianavyolingana baina ya majengo hayo mawili.
Pamoja na hayo chuo hicho Nabii Isaya humtaja Yesu kama Mungu mwenye nguvu Isaya 9:6-10 tendo ambalo linapingwa na Umma wa Kiislam hivi leo hivyo kamwe Sinagogi na Misikiti si Majengo yanayowiana katika tafsiri na pia hata katika matendo kadhaa makuu ya kiimani pamoja na kufanana kwa machache kama yale yahusuyo mavazi n.k.
KUMFANYA YESU NI MUISLAM NI MAKOSA.
Yesu alipaa kwenda mbinguni mwaka wa 31 kabla ya kuzaliwa kwa Mtume Muhamadi mwaka 570 (BK) ambaye ndiye muanzili wa Uislam.
Yesu hakufuata kamwe nguzo tano za Uislam na hata hivyo bado hapakuwa na nguzo hizo kwa kuwa muasisi wa imani ya Uislam yaani Muhamadi (SAW) hakuwepo.
Qur-an 12:20 aya hii inasimulia kisa cha kuuzwa kwa Yusufu kule Misri.
Lakini pamoja na hayo aya hiyo katika ufafanuzi wake uliotolewa na mfasiri chini yake unaonyesha kuwa Uislam ni dini aliyokuja nayo Mtume Muhammad na pia hata kipindi hicho cha Yusufu haukuwepo.
Hebu sasa tuchunguze nguzo hizo tano za uislam na kisha upime mwenyewe endapo Yesu alizitekeleza hizo ili kuwepo na usahihi kwa wanaofundisha na kudai kuwa Yesu alikuwa Muislam.
NGUZO (5) ZA UISLAM
1) Shahadat kushahadia- hili ni tendo la kukili kuwa
Mungu ni mmoja na Muhammad ni Mtume wake.
2) Ikhamu Swalat Kusimamisha swala- hili ni tendo la kufuata
Utaratibu wa kusali swala mara tano kwa siku.
3) Ita-U Zhakhati Kutoa zaka- kutoa mali kwaajili ya Masikini.
4) Swaum Shar Ramadhani Kufunga – hili ni tendo la kufunga kwa kuangalia
mwezi linalochukua muda wa siku 29,30
5) Hijat ila Baitu Llah Kuhiji Maka- hili ni tendo la ibada ya kwenda mji
wa Makka linalo ambatana na matukio
mbalimbali kama vile kupiga mawe Shetani na kuheshimu jiwe jeusi nk.
Je yesu alifanya hayo ili aitwe Muislam? Yesu kamwe hakuwa Muislam (Yasua Laysa Muslimuna)
Jifunze zaidi
Qur-an 6:14 Muhammad ni wakwanza katika wenye kusilimu
Qur-an 10:104 Uislam ni dini ya Muhammad
Swali;
Kwa kadri ya Muktadha wa aya hizo unajifunza nini unaposikia baadhi ya watu wakijenga hoja na kushikilia msimamo kuwa hata Bwana Yesu naye alikuwa Muislam?
Mungu akubariki unapo adhimu kuchukua jukumu la kuelimisha wengine juu ya ukweli huu.