HUDUMA YA INJILI NA
MAHUSIANO KWA WAISLAMU
Sura ya Kwanza
Amri na hukumu katika maandiko ya Qur-an na Biblia
------------------------------------------
Sura ya Pili
Siku ya Saba [Sabato] inavyoitwa katika Kiyunani,Kiarabu na Kiebrania
---------------------------------
Sura ya Tatu
Isemavyo Qur-an juu ya siku ya ibada ya kweli [Sabato]. Ni ljumaa, Jumamosi au Jumapili?
---------------------------------
Sura ya Nne
Nini chimbuko la ibada ya siku ya ljumaa ya Kiislamu? Na Je, inasimama mahala pa Sabato?
---------------------------------
Pr. Dominic Mapima
Muslim areas Evangelism Instructor.
Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com
SIKU YA KUABUDU (SABATO) YA KWELI KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA
3.Je! Yesu ni nani haswa?
Katika sehemu ya mwishoni sura ya 2 ya jarida hili nimezungumzia juu ya kuwepo kwa sifa zinazo mfanya Mwenyezi Mungu (Allah) kuitwa Mungu, na nikaeleza kuwa sifa hizo kamwe haziwezi kuwa za binadamu hebu tuone mifano michache ya tabia hizo ambazo:-
Communicable altibuties - tabia shirikishi
Un communicable altibuties - tabia zisizo shirikishi
Mungu umshirikisha Mwanadamu Ni za Mungu pekee
Tabia shirikishi Commucable altibuties
Tabia zisizo shirikishi Un communicable altibuties
Upendo Uumbaji
Amani Uweza
Furaha Umilele
Hakima Kuabudiwa/kutukuzwa
Utu wema Nuru ya Mbingu na Dunia
Maarifa Kuokoa
Mamlaka ya Mbingu na Dunia
Hivyo ili Mungu aitwe Mungu lazima awe na sifa ambazo kamwe Mwanadamu hawezi kuzifikia, hivyo basi ili kujua asili haswa ya Yesu na mamlaka yake ni vyema tuka fuatilia kwa makini kupitia tabia hizo, haswa zile zinazo mhusu Mungu pekee na kuchunguza kwa makini kuwa je! Yesu alikuwa nazo sifa hizo hata aitwe Mungu?
Pamoja na hayo ndugu msomaji wangu ninakuomba kuwa na moyo laini na wa ukubali kwa kadri maandiko yatakavyo zungumza na kubainisha ukweli haswa wa mada hii tata hebu sasa tuanze safari yetu taratibu na kwa uhakika ili tuweze kuvuna maarifa haya ya ajabu.
Je! Ni sifa zipi basi zimhusuzo Mungu, alizonazo Bwana Yesu? Je Qur-an na Biblia vinasema nini?
Sifa tutakazo zichunguza kwa muktasari.
(1) Uumbaji
(2) Mamlaka ya Mbingu na Dunia
(3) Kutukuzwa na viumbe vyote na
kusujudiwa
(4) Nuru ya Mbingu na ardhi
(5) Kuokoa
(6) Umilele
Hizo ndizo baadhi ya sifa tutakazo zipitia kwa makini ili zitusaidie kugundua ukweli haswa juu ya Bwana Yesu kuwa Je! Ni kweli anastahili kuitwa Mungu? Tutakubaliana ndugu msomaji wangu mpendwa kuwa sifa hizo zote nilizo zitaja ambazo ndizo tutakazo zipitia zote zinamhusu Mungu pekee na kamwe haziwezi kumhusu binadamu yeyote wakawaida vinginevyo kama yupo anaonekana ni binadamu lakini anasifa hizo basi atakuwa na asili inayopita ubinadamu alionao, maana hata Mungu anauwezo wa kuchukua mwonekano wowote hata ule usio eleza kabisa mamlaka yake ili kujifunua kwa watu wake.
Rejea “ Qur-an 20:9-11
Mungu alijifunua kwenye kijinga cha moto na kuongea na Musa
Hata malaika wa Mungu uweza kutwaa maumbile mbalimbali.
Soma” Qur-an 19:17 ………… Malaika akajimithilisha (kujibadili-kujifunua ) kwake kwa sura ya binadamu aliye kamili.
Pengine jambo hilo tutaliongelea zaidi mbele ya jarida hili la “Darubini ya Imani” katika mfululizo wa mada hii makini na yenye utata kwa watu wengi, zaidi sana wale wasio soma na kuchunguza maandiko kwa makini.
Hebu sasa kwa makini tuanze kuchunguza taratibu vigezo hivyo vya msingi katika mchakato wa mada hii.
(1,1) Uumbaji
Kwa ujumla Mungu yeye ni Mungu tu kwa asili kama alivyo Mungu, lakini sisi wanadamu tunavyo vigezo vinavyo tusaidia kumtambua katika kikomo chetu cha ufahamu wa kibinadamu hivyo moja kati ya sifa kuu zinazomtambulisha Mwenyezi Mungu kwetu ni tendo hili kuu “Uumbaji”.
Uumbaji umweleza Mungu vyema sana katika akili ya Mwanadamu (Ibn adam), kupitia tendo hili la uumbaji wanadamu hujifunza na kutambua kuwa:-
-
Mungu ndiye asili (Chanzo) ya vyote viijazavyo dunia.
-
Yeye kwa hakika ndiye asili na chanzo cha uzima maana yeye mwenyewe ni uzima.
-
Kuwepo kwetu kunatokana na kuwepo kwake kusiko na mwanzo wala mwisho
-
Yeye ndiye mwenye mamlaka juu ya maisha yetu awezaye kuyazuia au kuyaruhusu kuendelea, ni mwanzilishi ndiye mtoa uhai nasi tunaishi ndani yake.
Sifa na mamlaka hii kuu ihusuyo uumbaji kamwe haiwezi na wala haitoweza kumhusu mwanadamu wa asili ya Dunia hii, Mungu Mwenyewe alisema.
Isaya 42:8 “Mimi ni Bwana ndilo jina langu na utukufu wangu sitampa mtu mwingine wala sitawapa sanamu sifa zangu”
Vitabu vyote vya maandiko ya kidini uelezea kwa upana juu ya umaalumu wa sifa hii ya uumbaji ni vile isivyopaswa wala kustahili ya uungu hebu tufuatilie ushahidi wa kimaandiko haswa tukianza na mafunuo ya Qur-an pamoja na Biblia Takatifu na kisha tutaangalia kwa makini kuwa Je! Bwana Yesu anasifa hiyo ya uumbaji ili aitwe Mungu?
Uumbaji sifa ya Mungu Pekee.
Katika mafunuo ya Qur-an zipo habari kadha wa kadha na maelezo ya namna mbali mbali juu ya uumbaji, katika sehemu hii tutachunguza kwa makini ili kuweza kuona uzito na umakini wa tendo hili la Uumbaji na yakuwa ni nani pekee anaye husika na mwenye uwezo huo wa kuumba.
Muumbaji ni nani?
Qur-an surat Yunus 10:34 sema je (yuko)katika hao mnaomshirikisha Mwenyezi Mungu aliyeanzisha kuumba viumbe, kasha atavirejeshea? Sema “Mwenyezi Mungu ndiye aliye anzisha viumba kisha atavirejesha. Basi mmegeuziwa wapi? ………………
Andiko hilo kama lilivyoonekana kujieleza linaonyesha kuwa hakuna uwezekano kwa Mwanadamu Kuumba, na yakuwa ni Mungu pekee awezaye kuumba na kuhuwisha atahivyo tendo lolote la kumhusisha mwingine awaye yote katika sifa hiyo ya Uumbaji ni kujitenga na ukweli wa Mungu.
Katika sura nyingine ya Qur-an kuna maneno yanayo mwelezea Mungu kwa kauli inayosema “hakuna anaye fanana naye hata mmoja “
Qur-an Surat nnasi 114:4
Katika aya nyingine ndani ya mafunuo ya Qur-an bado huweka na kutia mkazo mkuu juu ya swala hili la Uumbaji namna linavyohusika na Mungu pekee, pamoja na hayo, Qur-an huonyesha kuwa kazi yeyote ihusuyo Kuumba hata nzi (mdudu mdogo) inahusika na Mungu maana ni uanzishaji wa kiumbe (uhai).
Qur-an surat Al-hajj 22:73 Enyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni, hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu hawawezi kuumba (hata) nzi ……………………………
Hivyo mkazo mkuu wa Aya hizo za Qur-an ni kuonyesha umakini na upekee wa tendo hilo linalo mfanya Mungu kuwa Mungu kwa watu wake, hivyo katika sehemu hii tutaangalia kwa makini kuwa Je! Kweli Bwana Yesu anaweza kuwa na sifa hiyo ya kuumba inayo onekana kwa mkazo mkubwa kuhusika na Mungu pekee?
Pamoja na Aya hizo za Qur-an pia tunaweza kuona Biblia nayo ikiweka mkazo juu ya umaalumu wa tendo hilo la Uumbaji, na yakuwatendo hilo na mengineyo yatendwayo na Mungu hulenga kufanya wanaadamu wamche Mungu kutokana na uwezo wake huo wa kiutendaji ambao kamwe hauwezi kufikiwa na mwanadamu.
Mhubiri 3:14 Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele, haiwezekani kuzidisha kitu, wala kupunguza kitu, nayo Mungu ameifanya ili watu wamche yeye.
Hapo Biblia inaonyesha wazi kuwa zipo kazi zinazohusika na kufanywa na Mungu (Aya 14- Kila kazi aifanyayo Mungu) bila shaka Biblia hapo hulenga kuonyesha kuwa kuna mambo kadha wa kadha ambayo kamwe hayapo chini ya uwezo wa binadamu maana awezaye kuyatenda ni Mungu pekee naye hamshirikishi mwanadamu.
Pia Biblia hutaja sababu zinazopelekea matendo hayo kuhusika na Mungu pekee nayo ni kuwa watu wamche Mungu pekee (ili watu wamche yeye) hivyo basi tendo hili la kuumba na mengineyo ya mhusuyo Mungu humfanya Mungu kustahili kuabudiwa.
Hebu tuone mkazo wa Aya nyingine.
Isaya 44:24 BWANA, Mkombozi wako, yeye aliye kuumba tumboni asema hivi, mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote: nizitandazaye mbingu peke yangu: niienezaye nchi ni nani aliye pamoja nami?
Ndugu msomaji wangu bado Biblia inaendelea kuonyesha umakini na upekee wa tendo hilo, hapo Biblia inafunua mambo yafuatayo:-
-
Vitu vyote vinavyoonekana ni matokeo ya kazi iliyofaywa na Mungu.
-
Kuwepo kwetu duniani kunatokana tendo la Uumbaji mkuu uliofanywa na Mungu
-
Tendo hilo la Uumbaji kamwe siyo tendo (tabia) shirikishi bali hutendwa na Mungu pekee (niienezaye nchi ni nani aliye pamoja nami? Rejea Isaya 44:24)
Hivyo yeyote anayeumba katika mfanano wa utendaji wa kiuungu kunahaja ya kumchunguza kwa makini ili kujua asili yake na mamlaka aliyonayo ni ya namna gani haswa.
Je Yesu (Isa ) anasifa ya Kuumba ili aitwe Mungu?
Qur-an 3:49 na atamfanya mtume kwa wana wa Israel awaambie nimekujieni na hoja kutoka kwa mola wenu ya kuwa “ninakuumbieni”katika udongo kama sura ya ndege kisha “nampulizia” mara anakuwa ndege kwa “Idhini” ya Mwenyezi Mungu …………
​
Ndugu mpendwa hivyo ndivyo qur-an inavyoeleza juu ya kile alichokifanya Isa Ibn Mariam, hapo kunajambo kuu na lakimsingi kwa wale wanao chunguza maandiko kwa makini na kutafakari.
Andiko hilo la Qur-an linaeleza kuwa Isa Ibn Mariam aliwaeleza watu wa taifa la Israeli mambo ya fuatayo.
-
Amewajia na hoja kutoka kwa mola (mbinguni)
-
Yakuwa anaouwezo wa kuumba kiumbe kwa udongo
-
Anao uwezo wa kukipa uhai hicho alichoumba na kukipulizia pumzi ya uhai.
Ndugu msomaji wangu bilashaka umeanza kufunguka masikio kupitia Aya hiyo yaQ-an katika Aya hiyo inaonekana orodha ya matendo makuu ambayo Bwana Yesu (Isa) anatangaza kuwa na uwezo wa kuyatenda bila shaka matendo hayo ikiwa umeyachunguza kwa makini, yanaonekana kuhusika na uwezo wa kiutendaji wa Mungu Mwenyezi, sasa hebu tufuatilie kwa makini.
Nukuu kwa muktasari Qur-an 3:49
​
a) Nakuambieni katika udongo kama sura ya ndege.
bila shaka tendo hili hufanana fikiri na kile alichofanya Mungu pindi aliokuwa akimuumba Adamu maandiko yanaonyesha kuwa Mungu alifinyanga udongo na kumuumba Adamu vivyo hivyo Isa (Yesu) nae anafanya Uumbaji kwa kufinyanga udongo kwa sura ya ndege.
Ref: Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamuumba mwanadamu kutoka katika udongo wa ardhi
Qur-an 22:5…… tulikuumbeni kwa udongo mzee wenu Nabii Adamu ………
Hivyo Yesu anafanya tendo la Uumbaji kwa hatua zinazo fanana fika na kile alichofanya Mungu (kufinyanga udongo).
b) Kisha nampulizia mara anakuwa ndege.
Ndugu mpendwa yawezekana liletendo la kufinyanga udongo lisiwe na nguvu sana kwa wajenga hoja , lakini hapa ndipo panapo nishangaza zaidi Qur-an inapoonyesha wazi kuwa Isa aliweza kupulizia udongo nao ukapata uzima na kuwa kiumbe hai.
Wanasansi huu ndio uumbaji na wanabaiolojia wamejitahidi kuumba na kutengeneza mtu lakini wamegonga mwamba inapofikia hatua ya kumfanya kuwa kiumbe hai, aweze Kutembea, Kunusa, kuona n.k
Lakini maandiko ya Qur-an ufunua siri hii ya ajabu, bilashaka tendo hili la kupuliza pumzi na kitu kikawa hai ndiyo uleta maana halisi ya Uumbaji na hili ndilo tendo linaloleta maana na uzito haswa unaofanya tendo hilo kuwa rasmi na kumhusu Mungu pekee.
Mafunuo ya Qur-an huonyesha kuwa tendo hilo haswa ndilo alilotenda Mungu alipokuwa akimuomba Adamu nalo ni tendo la kutoa uhai (Maisha) kwa kuomba.
Qur-an surat 15:27
Tunajua fika juu ya tabia ambazo Mungu umshirikisha mwanadamu na pamoja na hayo zipo zile ambazo Mungu kamwe hawezi kumshirikisha mwanadamu, lakini katika andiko hilo tunaona Yesu akitenda kazi hiyo kuu yenye uhusiano kwa asilimia miamoja na uwezo wa Kiuungu bilashaka huyo Yesu anayo asili inayopita ubinadamu aliokuwa nao na siyo asili ya kawaida.
Je! Mbona Qur-an inasema aliumba kwa idhini ya Mungu?
Inawezekana ndugu msomaji wangu ukawa na swali la namna hiyo ndani ya moyo wako hebu niruhusu sasa niweze kuondoa mashaka uliyonayo.
Je! Neno kwa idhini humaanisha nini?
Katika tafsiri ya kawaida Neno “Idhini” humaanisha “ruhusa” au “Ukubali”
Hivyo Qur-an inapomnukuu Nabii Isa akisema kwa “idhini” inaleta maana tu ya ukubali, ruhusa toka kwa Mungu.
Swali:- je kwanini apewe ruhusa na hali yeye ni Mungu? Au Je kuna miungu wangapi?
Jibu:- katika mafunuo ya Biblia mara kadhaa Bwana Yesu ametumia kauli hiyo ya kuruhusiwa au kukubaliwa na Mungu (eg: Yohana 5:30) mara kadhaa Yesu alisema “ninenalo si neni yaliyoyangu nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo”
Kwanini aseme hivyo (kwa idhini)?
Kwa msingi ujio wa Yesu hapa Duniani ulimlazimu kufunika uwezo na mamlaka yake ya asili ya Kimungu, ilimpasa kumwelekeza mwanadamu kwa vielelezo hai vya kimwenendo, hali na mazingira hayo yalimfanya kujipa cheo cha chini mara kadhaa alipozumngumza na watu.
Rejea Qur-an 20:9-11 Mungu alijifunua kwa Musa kupitia kichaka cha moto bila shaka alichukua ufinyu huo ili kuwa Asili na mwanadamu.
​
Pamoja na hayo Bwana Yesu akuadhimu mara chache kufunua taratibu mamlaka aliyonayo kiasili, mfano ni pale aliposema.
Yohana 10:30 mimi na Baba tu umoja.
Kauli hiyo iliwafunulia mafarisayo juu ya mamlaka ya Yesu ya Kimungu, lakini haikuwa jambo rahisi kwao kukubaliana na hilo
na katika aya hiyo tunaona wakiadhimu kumpiga mawe kwa kujiita yeye ni Mungu.
Bilashaka Yesu alitambua saikolojia ya imani ya watu hao anaowajua hata mioyo, hivyo Yesu aliamua kushuka kwa kumtaja Mungu wanayemdhani kama Mungu aliye ng’ang’ana Mbinguni tu lakini kwa hakika hiyo ndiyo asili yake binafsi.
Ndiyo maana alisema kwa Idhini.
Katika wazo hilohilo ndiyo maana Yesu Utumia neno kwa “Idhini”alipenda watu watambue mamlaka yake katika utendaji wake zaidi kuliko katika maneno yake
Hata hivyo neno kwa “Idhini” halimaanishi kwa “uwezo” Idhini na uwezo ni mambo mawili yanayo tofautiana sana
Mfano:- wewe unaweza kupewa Idhini ya kuhubiri lakini usiweze (usiwe na uwezo ) wa kuhubiri hivyo idhini( ruhusa ) na uwezo nitofauti kulingana na maandiko tabia ya Yesu ihusuyo Uumbaji uonekana akiwa nayo katika asili (Yohana 1:1-3) hivyo ni tabia ya kiuwezo na mamlaka yake ya Kimbinguni kabla ya kujishusha na kuvaa ubinadamu (nitalieleza mbele kwaupana ) na kuja hapa duniani.
Neno idhini Isa (Yesu) analitumia anapo kuwa hapa Duniani kama sehemu ya hatua yake ya kujishusha na kutwaa ubinadamu kwaajili ya kuokoa, lakini bado tendo la uumbaji linarejea asili na mamlaka yake kama Muumbaji na si wa ndege tu bali Dunia kwa ujumla (Yohana 1:1-3)
Qur-an inampa cheo gani Yesu (Isa) kwa tendo la Kuumba?
Uandishi au kuchapaji mwandishi na mengineyo ya kimsingi.
Qur-an 16:17 …….Ati yeye aliyeumba (naye ni Mwenyezi Mungu ) atakuwa sawa na wale wasio umba je hamkumbuki?
​
Andiko hilo la Qur-an linasema kuwa
- “Ati yeye aliyeumba (Mungu) atakuwa sawa na wasio umba”?
Jibu :- la” aliyeumba hawezi kuwa sawa wasioumba bali aliye umba anakuwa sawa na aliyeumba hivyo ikiwa Yesu aliumba je yeye ni nani?
Qur-an kamwe haimpi sifa au usawa kiumbe yeyote asiye na sifa inayohusika na Mungu, maana sifa inayomhusu Mungu haswa ile ya kuumba ndiyo humfanya Mungu kuitwa Mungu kamwe hawezi kupewa Mwanadamu.
Pamoja na hayo jambo la kushangaza ni pale Qur-an inapoo nekana kuweka wazi kuwa Nabii “Isa Ibn Mariam” naye alikuwa na sifa hiyo inayo mhusu Mungu maana naye aliweza kuumba
(rejea neno nakuumieni Qur-an 3:49)
Na kutokana na kile kichosemwa na aya tuliyoisoma punde Nabii Isa anaonekana kuwa sawa na Mungu au kwa lugha rahisi naya ufupi yeye ni Mungu Muumbaji aliye adhimu kuvaa ubinadamu, lakini ana mamlaka inapita huo ubinadamu (yeye ni neno, muumbaji).
(2,2) Mamlaka ya Mbingu na Dunia
Baada ya kuona sifa hiyo ya kwanza ya Mungu ihusuyo Uumbaji ambapo tumeona wazi vile ambavyo Bwana Yesu anavyohudika nayo, nivyema sasa tukaenelea na mchakato huu wa mada hii yeye utata kwa kuangalia kigezo cha pili kihusucho mamlaka ili kuendelea kuona kama bwana Yesu anayo mamlaka hiyo ikiwa yeye ni Mungu?
Mamlaka ni kitu gani?
Kwa ufupi mamlaka huashiria hali ya kiutawala anayokuwa nayo mtu juu ya eneo sehemu au mazingira fulani, hali hiyo humpa mtu huyo uwezo wa kuamua na kuongoza pasipo kikwazo mwingine awayeyote.
Moja kati ya sifa zimhusuzo Mungu ni tendo hili la kuwa na mamlaka juu ya mbingu na Dunia niwazi kuwa hakuna kiumbe yeyote asiye na sifa ya kimungu anayeweza kuwa na mamlaka juu ya Mbingu na Dunia, sifa hii kama ilivyo ile ya kuumba uhusika na Mungu Mwenyewe.
Kuashiria kuwa hii ni mamlaka ya Mwenyezi Mungu pekee tunaweza kuona mifano ya wanadamu wa kawaida waliojaribu kujifanya kuwa nao wanamamlaka kile kilichowapata baada ya tendo hilo.
Mfalme Nebkadneza – mfalme huyo alifanyakazi ya kuujenga mji wa ………………
Na baada ya kujenga vyema kwa kuweka mabustani ya angani n.k. alijisikia kiburi na kudai kuwa ndiye mwenye mamlaka na muumba wa mji huo, tendo hilo halikuwa jema machoni pa mwenye mamlaka halisi yaani Mungu.
Kama matokeo ya kufuru hiyo ya wizi wa mamlaka na uwezo wa Kimungu Mfalme hivyo aliambulia…………………
Lakini tunaposoma ndani ya Biblia hiyohiyo, maandiko Matakatifu ya Biblia yanapo mzungumzia Bwana Yesu sehemu kadhaa huonyesha vile alivyo kuwa na mamlaka sehemu ya maandiko kama:
Mathayo 28:19-2 Bwana Yesu mwenyewe anatamka
“Nimepewa mamlaka yote Mbinguni na Duniani”
Sehemu nyingine ni katika mafunuo ya Qur-an yenyewe katika maneno yasiyo fanana sana na hayo ya Kibiblia lakini nayo inaonyesha upekee aliokuwa nao Yesu (Isa bin Mariam )
​
Hebu fuatialia aya ifuatayo:-
Qur-an 3:45 ………. Mwenyezi Mungu anakupa habari njema ya “Neno” litokalo kwake
Jina lake ni Masihi Isa Mwana wa Mariam – mwenye “heshima” katika “Dunia” na “akhera” …………
Qur-an hapo inataja ninaouona ni upekee au mamlaka ya Bwana Yesu pale inapoeleza kuwa ana “heshma” katika “Dunia na Akhera”. Katika Qur-an ni marachache kuona mtu yeyote tu akielezwa katika namna kama hiyo …………..
Hilo linaonyesha kuwa kuna upekee na kitu cha ziada kinacho pelekea sifa hizi kuu za kimamlaka kuangukia kwa Bwana Yesu …………… na kama tulivyoona yeye kwa hakika ni Mungu.
​
​
​