top of page
99-997235_eid-mubarak-mosque-png.png
THREE ANGELS MINISTRY OFFICIAL LOGO.png

HUDUMA YA INJILI NA

MAHUSIANO KWA WAISLAMU

mizani ya haki.png
Yaliyomo

Sura ya Kwanza

Amri na hukumu katika maandiko ya Qur-an na Biblia

------------------------------------------

Sura ya Pili

Siku ya Saba [Sabato] inavyoitwa katika Kiyunani,Kiarabu na Kiebrania

---------------------------------

Sura ya Tatu

Isemavyo Qur-an juu ya siku ya ibada ya kweli [Sabato]. Ni ljumaa, Jumamosi au Jumapili?

---------------------------------

Sura ya Nne

Nini chimbuko la ibada ya siku ya ljumaa ya Kiislamu? Na Je, inasimama mahala pa Sabato?

---------------------------------

Vitabu vya Chambuzi Mbalimbali
vlcsnap-2019-10-23-10h10m27s610.png

Pr. Dominic Mapima

Muslim areas Evangelism Instructor.

Mobile: 0754-527143

Email: dominicmapima@yahoo.com

practices-rotator.jpg

  SIKU YA KUABUDU (SABATO) YA KWELI KWA MUJIBU                             WA QURAN NA BIBLIA                            

3. Isemavyo Qur-an juu ya siku ya ibada ya kweli [Sabato]. Ni ljumaa, Jumamosi au Jumapili?

Ndugu msomaJi wangu mpendwa, baada ya utangulizi huo wa nyuma sasa

nikuombe kuwa makini zaidi tunapoingia kwa ndani zaidi katika kiini cha mada hii yenye utata mkubwa.

 

Na hapa tunahitaji kuchunguza kwa undani zaidi katika mafunuo ya Qur-an ili kuvuna maarifa haya mapyajuu ya vile Qur-an inavyoeleza kuhusu ibada hii ya siku ya saba [Sabato] napia tutaona na kuiuliza Qur-an iweze kuweka wazi siku hiyo kuwa ni siku gani katika mfululizo wa siku za juma yaani Jumatatu, Jumanne- Jumatano, Alhamisi, ljumaa, Jumamosi na Jumapili, Je ni ipi inayokusudiwa kama siku ya Saba iliyo ya tangu awali ambayo ndiyo hasa siku ya kweli ya Ibada na kustarehe kama mungu mwenyewe alivyoonyesha kielelezo kwa kustarehe katika siku hiyo.

 

Je! ni siku gani iliyo ya saba (Sabato) katika siku za wiki! ljumaa, Jumamosi au Jumapili? Maandiko ya Qur-an yatatoa uchambuzi.

​

Nijambo linaloeleweka na kukubalika na jamii ya Kiislam kuwa; jamii kubwa ya watu waliomlea na kupenda mtume muhamadi ili kuwa ni ya watu wa imani ya Ukristo- vitabu mbali mbali vya Kiislam huweka wazi hata baadhi ya marafiki walio kuwa karibu na Muhamadi ambao walikuwa ni Wayahudi wa dini ya Kikristo (nasara) kama vile:-

 

*     Waraga bin Naufal

 

*     Bwana Jabil

 

*     Binti Maria (Mke wa Muhamadi wa Kiyahudi) n.k

​

Hivyo ndugu msomaji ukaribu huo wa Muhamadi na watu hao ambao baadhi

yao walikuwa ni watu wa dini sahihi za Kiyahudi na watunzaji wa siku ya kweli ya Ibada [Sabato], ndiyo uliomwezesha Muhamadi kueleza vyema Juuya ukweli wa siku hii ya ibada ya Sabato. Kama tutakavyoona.

 

Hata hivyo Mtume Muhamadi mwenyewe alikuwa na misafara ya kibiashara ya

chumvi, ambayo ilimpa nafasi ya kufika maeneo ya Shamu (Syria) pamoja na mji wa Yerusalem, bila shaka Muhamadi aliweza kupata habari nyingi kuhusu imani ya Kikristo (naswara) na sasa hebu tuone namna ilivyozungumzia juu ya Ibada hii ya kweli ya siku ya saba ya juma yaani Sabato na je? ni siku gani hasa!

 

Kama tulivyoona Qur-an inakubaliana na mpango wa uumbaji katika siku sita na kuwepo kwa siku ya saba ambavyo Mungu alistarehe kama tulivyosoma katika;-

 

Qur-an A araf  7:54 Mola wenu ni mwenyezi mungu aliyeziumba mbingu

                    na ardhi kwa siku sita kisha akatawala katika arshi

                    yake.

 

 

Hebu sasa twende mbele zaidi, ili tuweze kuifahamu hasa siku hiyo ambayo mwenyezi mungu hakufanya kazi yeyote maandiko ya Qur-an yataendelea kutusaidia katika Jambo hili-

 

Qur-an Surat A-NISAA 4:154 na tukanyanyua mlima juu yao[hao

                          Mayahudi] kwa kufanya Agano nao [la kufuata

                          taurat] na tuliwaambia"Liingieni lango [la

                          nchi ya shamu]" hali ya kuinama {kama

                          mnafukuu] [wakapinga]. Na [pia] tukawaambia;

                         "msiruke mipaka kwa [kuvunja taadhima ya]

                          Jumamosi" na tukachukua ahadi iliyo madhubuti

                          kwa mambo hayo na mengineyo wala wasitimize.

​

Ndugu mpendwa msomaji hebu tuwesambamba kuichunguza aya hiyo,

hapa tunapata mambo makuu matatu na kwa uwazi ndipo tunapoweza

kugundua ukweli juu ya siku hiyo iitwayo Sabato kuwa ni siku ipi kati ya siku zetu za wiki.

​

Mambo makuu matatu tunayo ng'amua katika aya hiyo-

  1. Mungu aliweka Agano maalum kwawatu wakale [Aganoni makubaliano],

 

2. Agano lenyewe lilihusika na namna ya kuingia shamu na kutunza siku ya kweli ya fbada aiTibayo Qur-an hapo imclaja kwa wa/i kuwa kumbe inaitwa Jumamosi [Sabato]

 

3. Ahadi hiyo haikuwa ya mzaha [ni ahadi madhubuti] lakini waliivunja.

 

Mpendwa tumaini langu lilikuwa ni kuu nilipokuambia kuwa Qur-an itatoa

Majibu juu ya siku hii kuwa ni ljumaa, Jumapili au Jumamosi! Na hapa tumevuna maarifa ya wazi juu ya ukweli hasa wa siku hiyo kuwa ni siku ya Jumamosi.

 

Hivyo rafiki yangu uliyeshikilia kitabu hiki hayo ni maarifa ya wazi na

rahisi ikiwa ni muislam au mkristo- siku ya saba inayozungumziiwa na Qur-an tukufu ni siku ya Jumamosi na si vinginevyo, lakini ikiwa umuislam ninafikiri kwenda ulitarajia kuona kuwa siku hiyo yaweza kuwa ni ljumaa ambayo waislam hukutana na kuswali swala ya Jamaa, hilo tutalitazama kwa kina sana mbele zaidi katika kurasa za kitabu hiki cha maarifa mapya hebu tuendelee kuchunguza

zaidi juu ya ukweli hasa wa siku hii ya Jumamosi kama siku ya Ibada,

 

Je! mahesabu ya siku hayakupotezwa?

 

Hilo linaweza kuwa swali lako mpendwa msomaji, na yafuatayo ni majibu ya mashaka yako..

 

Kwa kawaida na ukweli [bil-haq] Mwenyezi Mungu hupenda kuhakikisha kuwa chochote alichokianzisha kinadumu na kulindwa hadi mwisho na ndivyo ninavyoweza kukuhakishia kuwa Mungu alilinda siku hii ya saba maana yeye ndiye aliyeianzisha. kulinda huko si kwa njia tuzifahamuzo, bali alitoa ujuzi na vipawa kwa wanadamu ili waweze kujua namna ya kuhesabu majira na saa na hivyo isingeliwezekana kusahau au kupoteza siku hii ya ibada ya Bwana [Sabato] hebu na tuone mifano kadhaa:-

 

Tangu zamani watu walihesabu masaa na mizunguko ya siku kwa kutumia Solar Calender [Kalenda ya jua] na walifaulu vizuri hivyo kutopoteza siku au mwenendo wa masaa. 

​

Pia njia ya kwanza inadaiwa ilikuwa ikitumika miaka ya 350 kabla ya kristo na ilikuwa ni ya kufuata kivuli cha binadamu kinavyosogea kufuata mwanga wa jua.

 

Katika karne ya nane [8] saa kongwe ilitumika huko Misri na ingali imehifadhiwa hata leo katika jumba kongwe.

 

Karne ya kumi na nane [18] mjapani aitwaye Lntern Clocic aligundua saa inayo tumia mashine na mashine hiyo iliitwa Harogium kabia ya kuitwa Clock.

​

Mpendwa msomaji wangu je umeona vile mungu alivyoibua vipawa na hivyo

kufanya mahesabu ya siku kutoharibikiwa? Hivyo ni wazi kuwa siku ya saba inabaki kuwa ni Jumamosi na si siku nyingine yeyote, kumbuka Muhamadi aliishi zama na mbele Sana baada ya Yesu Kristo yaani.

 

• Yesu alipaa mwaka wa 31

 

• Mohamadi alikuja mwaka 570 Baada ya Kristo

 

Pamoja na kipindi chote kupita kati ya mtume Muhammad na Yesu Kristo, pamoja na manabii wengi wa Kibiblia. lakini tunaona Muhamadi akitangazia Dunia kuwa siku ya saba [Sabato] ni siku ya Jumamosi na siyo vinginevyo. pamoja na hayo kalenda maalumu ya kiarabu nayo huweka wazi juu ya ukweli huu wa siku sahihi iliyo Sabato (siku ya saba)

 

Hebu tuone mpango wa siku hizo za juma na ziitwavyo katika kalenda hiyo ya kiarabu.

​

Kiarabu                                            Kingereza                                            Kiswahili

​

Yawm L-wahid                                   Sunday                                               Jumapili

Yawm L-ithnain                                  Monday                                              Jumatatu

Yawm - Thalathat                               Tuesday                                              jumanne

Yaum - Rabi-u                                    Wednesday                                        Jumatano

Yawm L-Khamsy                                Thursday                                            Alhamisi

Yawm L-Jamaa                                   Friday                                                ljumaa

Yawm L-sabt                                       Saturday                                            Jumamosi

​

Ndugu msomaji hivyo ndivyo kalenda iliyoandikwa na waarabu inavyoonyesha, kama tunavyoona kalenda hii huanza kwa kutaja siku ya kwanza yaani Jumapili na siku ya ljumaa huwekwa wazi kuwa ni siku ya sita na hivyo siku ya Jumamosi hubaki katika nafasi yake sahihi kama siku ya saba.

 

Baada ya uchambuzi huo hebu sasa na tuendelee tukiwa na uhakika tele na

hivyo Qur-an inaweza kuchukua vyema nafasi yake ili kutupa habari zaidi juu ya umakini wa siku hii ya Sabato (Jumamosi) ndani ya Qur-an yako mambo makuu yaliyo nenwa humo kuhusiana na siku hii ya Sabato, sitakosea nikikuhakikishia ndugu msomaji kuwa Ibada ya siku hii ya Sabato ndiyo iliyo na makazo kuliko ibada zote ndani ya maandiko ya Qur-an.

 

 

Katika uchambuzi huu. tutapitia kwa makini jumla ya aya zipatazo nne zinazo Zungumzia Juu ya Ibada hii sahihi ya Sabato (Jumamosi) na kupitia maandiko hayo tutaona kuwa Je Ibada hiyo ingali inadumu hata hivi leo au iliishia zamani?

 

Kama nilivyotangulia kueleza hapo nyuma. kuwa kitabu cha Qur-an huinua na kuieleza ibada hii ya siku ya saba (Sabato) kuliko ibada nyingine yeyote ndani maandiko yake.

 

Hebu sasa tuzichunguze aya hizo zipatazo nne; iii kujivunia maarifa haya juu ya ukweli kuhusu siku haswaa iliyo ya kweli ya ibada,

 

Qur-an 7:163-164 Na waulizeni habari za mji amhao ulikuwa kando

                ya bahari [watu wa mji huo] walipokuwa wakivunja

                [sheria ya] Jumamosi [ambayo waliambiwa wasifanye kazi

                katika siku hiyo, wafanye ibada tu, na kazi yao ilikuwa

                uvuvi] Samaki wao walipowajia juu juu siku za jumamosi

                zao, na siku isiyokuwa jumamosi hawakuwa wakiwajia

                [hivyo] Basi namna hivyo tuliwatia mtihani kwa sababu

                ya kiasi kwao.

 

Ndugu mpendwa msomaji wa kitabu hiki cha maarifa mapya, unaweza kuona

aya hiyo ya Qur-an ikianza kuonyesha umuhimu wa siku hiyo ya Sabato

(Jumamosi). Qur-an hapo inaweka wazi kuwa Mungu kamwe hakutaka

Mwanadamu kuivunja siku hiyo.

 

Tunaweza kuona onyo likitolewa kwa wavuvi hao, kuhakikisha kuwa hawavui

katika siku hiyo ya Sabato, na unapoendelea na aya hiyo unaweza kuona Mungu akiwatumia watu wengine kuwaendea wavuvi hao ili kuwapa onyo, kuwa wangekutana na adhabu ikiwa wangeliendelea kukaidi amri hiyo.

 

Mambo Makuu matatu [3] tunaweza kuyagundua kupitia aya hiyo

kuhusiana na siku hii ya Sabato.

 

-     Sabato ni amri ya Mungu inayopaswa kuwa sehemu ya tabia ya Mwanadamu katika kuiheshimu na kuitunza.

 

-     Kuivunja Sabato ni kuasi sehemu ya amri [sheria] za Mungu, na pamoja na hayo ilistahili adhabu kwa mtu huyo aliyeasi.

 

-     Watu wengine wanaodumu kutunza amri za Mungu, wanawajibika

kuwakumbusha wengine wanao asi au kulegalega katika kuishia tabia ya Mungu [Amri kumi].

 

Hayo ndiyo mambo ya pekee tunayoweza kujifunza kupitia ushahidi huo wa

maandiko ya Qur-an na bado tunaweza kusonga mbele ili kuendelea kuona

umuhimu wa siku hii ya Sabato kupitia aya hizo za Qur-an. na sasa hebu tuone ushahidi mwingine unaonyesha mkazo wa siku hii ya ibada [Sabato]

 

Qur-an 16:124 Hakika [adhabu ya kuvunja taadhima ya] Jumamosi

              Iliwekwa juu ya wale waliohitilafiana kwa ajili ya hiyo

              (Jumamosi) na kwa yakini mola wako atahukumu baina yao

              siku ya kiama katika yale waliokuwa wakihitilafiana.

 

Haya ndugu msomaji wangu! Hizo ni habari nyingine tena, hapo Qur-an

inaonyesha kuwa wako watu waliowahi kuasi siku hii ya ibada ya Jumamosi

[Sabato] na tunaambiwa kuwa adhabu iliwekwa juu yao.

 

PamoJa na hayo Qur-an inaonyesha kuwa watu hao walihitilafiana, tendo hili la kuhitilafiana ndilo linalo tusumbua hivi leo lakini tunachoshukuru ni kuwa kitabu cha Qur-an kilisha ona hayo tangu awali na zaidi ya yote.

 

Mungu atahukumu juu ya hilo siku ya kiama na hukumu inayotajwa hapo

inahusiana na wale waliosimama upande wa upinzani dhidi ya amri hiyo ya

wazi ihusuyo siku ya Ibada na mengineyo yaliyoelekezwa na Mungu.

 

Pamoja na hayo, kupitia aya hiyo na ile tuliyotangulia kuisoma awali, tunaweza kujiuliza maswali yafuatayo:-

 

1. Kwa nini Mungu alikuwa makini sana kuilinda siku hii ya Sabato?

 

2. Ikiwa watu wahadhibiwa kwa sababu ya kuvunja siku hii ya Ibada, Je kuna ukweli wowote kuwa Mungu aliiona si ya maana tena mbeleni?

 

3. Je! kwanini hatuoni ibada ya siku ya ljumaa n.k ikiwa na uzito kama huo wa siku hii ya Jumamosi.

 

Wakati tukijiuliza maswali hayo hebu tuzidi kuangalia aya nyingine za Qur-an ili kupanua maarifa hayo juu ya siku halisi ya Ibada,

 

Qur-an 4:47 Enyi mliopewa kitabu! Aminini tuliyoyateremsha

            yanayosadikisha yale yaliyo nanyi, kabla hatujazigeuza

            nyuso zenu tukuzipeleka kisogoni, au kabla ya kuwalaani

            kama tulivyo walaani watu [walioharibu utukufu] wa Jumamosi

            na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima kufanywa.

 

Binafsi ninashukuru sana kuwepo kwa kitabu cha Qur-an, maana ni kitabu kinachosema ukweli wake bila kupindapinda kama wanavyopinda wanadamu hivi leo.

 

Pamoja na kwamba maelezo mengine ya Qur-an hatuwezi kuyaona katika maneno va kibiblia. ila bado yanafaa kuwa ubao wa kufundishia kwa wale wenye miyoyo migumu.

 

Andiko tulilosoma punde linaonyesha kulaaniwa kwa baadhi ya watu kipindi cha nyuma kwa kosa la kuvunja Sabato, na hicho kimetumika kama kielelezo cha adhabu ya kukosa utii katika mambo matakatifu ya Mwenyezi Mungu.

 

Watu wa zama hizi tunatakiwa kujifunza umuhimu wa kutii maagizo ya Mungu, ili tusikumbane na hasira yake, yawezekana usilaaniwe hapa duniani, ila kuna kuitazamia adhabu katika siku ya hukumu ya Kiyama

 

Ibada ya siku hii ya kweli Sabato (Jumamosi) ina mkazo mkubwa ndani ya kitabu cha Qur-an anza kuitazama upya, na kuchunguza maandiko ili kupata ukweli huu wa maarifa mapya.

 

Maneno va ajabu yanayoinua ibada ya kweli ya siku ya Sabato [Jumamosi] ndani va Qur-an.

 

Qur-an 2:65 Na kwa yakini mmekwisha kujua (Khabari za) wale walio asi

            miongoni mwenu katika (amri ya kuiheshimu) Jumamosi Basi

            tukawaambia [Kuweni Manyani wadhalilifu) "

 

 

Mpendwa mimi binafsi aya hii ya Qur-an huwa inanishangaza na kunipa tafakari ya pekee juu ya uzito wa siku hii ya Sabato (Jumamosi). Kama tuonavyo aya hii ikieleza juu ya jamii ya watu fulani walioasi kwa tendo la kuvunja amri hii ya ibada ya kweli ya siku ya Sabato

(Jumamosi).

​

Pamoja na hayo Qur-an inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu aliwafananisha watu hao na nyani tena nyani wadhalilifu,

 

mambo ya kujiuliza

 

-     Kuna siri na uzito gani katika siku hii ya Jumamosi (Sabato) hadi Mungu afikie hatua ya kuwaita viumbe wake sawa na nyani hati sababu ameasi siku hiyo?

 

-     Nini hasa sababu ya Mungu kuwafananisha watu wake na nyani

tena nyani wadhalilifu?

 

-     Mimi binafsi ninachojua ni kuwa siku hii ya ibada (ya Sabato) ilitolewa na Mungu yeye mwenyewe na ni kati ya amri zake kumi alizoziandika kwa kidole chake mwenyewe na siyo

kuandikwa na Mwanadamu.

 

-     Kutokana na uzito huo ndugu msomaji wangu ni hakika Mungu Asinge vumilia kuona mwanadamu akichezea na kukaidi mambo hayo malakatifu

 

Qur-an inaripoti kuwa Mwenyezi Mungu aliwafananisha watu hao walioharibu amri ile ya siku ya Ibada sawa na nyani, kimsingi nyani hueleza tabia ya mtu asiye na msimamo katika jamho moja la kimsingi, kama vile ilivyo tabia ya nyani ya kuruka kila upande wa miti.

 

-     Mpendwa msomaji wangu, Sabato (Jumamosi) ndiyo siku haswa iliyowekwa na Mungu kama siku ya mikutaniko mikuu ya kiibada kama vilie Maandiko ya vitabu vyote vya Dini yalivyo weka wazi jambo hili kama tulivyoona.

 

-     Lakini pamoja na hayo bado swali linaweza kuwa, Je! siku ya Ijumaa ilitoka wapi sasa! Fuatilia uchambuzi huu katika sura ya nne ya kitabu hiki.

​

​

​

bottom of page