HUDUMA YA INJILI NA
MAHUSIANO KWA WAISLAMU
Sura ya Kwanza
Amri na hukumu katika maandiko ya Qur-an na Biblia
------------------------------------------
Sura ya Pili
Siku ya Saba [Sabato] inavyoitwa katika Kiyunani,Kiarabu na Kiebrania
---------------------------------
Sura ya Tatu
Isemavyo Qur-an juu ya siku ya ibada ya kweli [Sabato]. Ni ljumaa, Jumamosi au Jumapili?
---------------------------------
Sura ya Nne
Nini chimbuko la ibada ya siku ya ljumaa ya Kiislamu? Na Je, inasimama mahala pa Sabato?
---------------------------------
Pr. Dominic Mapima
Muslim areas Evangelism Instructor.
Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com
SIKU YA KUABUDU (SABATO) YA KWELI KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA
2. Siku ya Saba [Sabato] inavyoitwa katika Kiyunani,Kiarabu na Kiebrania
Ndugu mpendwa msomaji, neno hili Sabato hutumika katika misemo na lugha
mbalimbali za asili za kibiblia na hapa tunaweza kuona vile watu waliosema lugha kama Kiebrania na Kiyunani pamoja na Kiarabu walitamkaje neno hili Sabato, na lilileta maana gani:-
* Waebrania huita - Shabath
* Wayunani huita - Sabaton
* Waarabu huita -.Sabti
Matamshi haya yote pamoja na utofauti wake hutupatia maana moja tu nayo ni pumziko (rest) au kustarehe, na neno hili chanzo chake halisi ni mungu mwenyewe katika pumziko lake la siku ya saba ambayo hakufanya kazi yeyote (alistarehe - Sabato)
- Qur-an 7:54 –kisha akastarehe katika arshi .………….
- Mwanw 2: ]-4 - Bwana akastarehe siku ya saba.
Pamoja na hayo neno lenyewe Sabato huleta maana tu ya kustarehe [pumziko] hivyo ni rahisi tu mtu kujichagulia siku yake na kuiita Sabato, lakini jambo kuu ni kuwa bahati mbaya haitakuwa sawa na Sabato ile yenye maana ya siku ya saba katika siku za juma, ambayo mahasisi na mteuzi wake ni Allah (mwenyezi mungu) na siyo binadamu-
Kwa hakika mwanzo huo ndiyo utoa imani na ujasin kwa baadhi ya dini na
madhehebu kuweka siku zao za ibada, kwa kudai kuwa nazo huwcza kuwa Sabato tu - kumbuka mambo yafuatayo:-
a. Sabato ya siku ya saba ilifunuliwa na kuhasisiwa na mungu mwenyewe kama Qur-an na Biblia visemavyo.
b. Sabato ya siku ya saba imekazwa na kutiwa mhuri na Mungu mwenyewe
maana ndiye aliyeiandika kwa kidole chake mwenyewe kati ya amri kumi (Qur-an 7:'144 - 145. Kutoka 31:18)
c. Sabato ya siku ya saba hutangaza ushindi wa Bwana katika ukomo wa
uumbaji na kuzaliwa kwa Dunia, kama kumbukumbu yako ya kuzaliwa.