HUDUMA YA INJILI NA
MAHUSIANO KWA WAISLAMU
Sura ya Kwanza
Amri na hukumu katika maandiko ya Qur-an na Biblia
------------------------------------------
Sura ya Pili
Siku ya Saba [Sabato] inavyoitwa katika Kiyunani,Kiarabu na Kiebrania
---------------------------------
Sura ya Tatu
Isemavyo Qur-an juu ya siku ya ibada ya kweli [Sabato]. Ni ljumaa, Jumamosi au Jumapili?
---------------------------------
Sura ya Nne
Nini chimbuko la ibada ya siku ya ljumaa ya Kiislamu? Na Je, inasimama mahala pa Sabato?
---------------------------------
Pr. Dominic Mapima
Muslim areas Evangelism Instructor.
Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com
SIKU YA KUABUDU (SABATO) YA KWELI KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA
1. Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu
Kama inavyoeleweka katika historia, Bwana Yesu ni mmoja kati ya watu mashuhuri walio wahi kuishi katika ulimwengu huu, pengine Bwana Yesu anaonekana kuwa na mvuto mkubwa zaidi katika historia ya kidini na hata ya kidunia. Mvuto huo wa Bwana Yesu unatokana na mambo makuu ya ajabu na ya kustaajabisha aliyo yatenda katika dunia hii wakati wa kipindi cha maisha yake ya kumkomboa mwanadamu.
Umashuhuri wa kiongozi huyu wa Kidini umepelekea watu mbalimbali wa madhebu ya dini kumgombania na kila mmoja akitaka kuitwa kwa jina lake (mfuasi wa Yesu). Hali hiyo imepelekea kuzalika kwa mitazamo mbalimbali inayo lenga kumwelezea kiongozi huyo haswa juu ya mamlaka aliyokuwa nayo kiasili. Mitazamo hiyo pia inaonekana kugongana kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na uelewa wa uchambuzi wa kimaandiko unaonekana kutofautiana na hivyo kuleta migongano hiyo. Hebu tutumie fursa hii kuangalia mitazamo hiyo mbalimbali ya madhehebu juu ya Bwana Yesu.
Jehova’s Witnesess
Hili ni dhehebu lililoanzishwa na Ndugu Charles Taze Russel dhehebu hili huzalisha majarida mbalimbali chini ya kitengo chake cha uchapaji kiitwacho Watch tower Bible and tract Society kitengo hiki kinatoa majarida mbalimbali ambayo ndiyo yanayo elezea imani na mtazamo wa dhehebu hili juu ya Bwana Yesu dhehebu hili humwelezea Yesu kama kiumbe tu wa Mungu aliyepewa upendeleo kwa kuumbwa kabla ya kiumbe yeyote mwingine (mzaliwa wa kwanza ) nao hudai kuwa Bwana yesu husimama kimamlaka katikati ya viumbe na Mungu lakini kamwe hana mamlaka ya kiasili ya Uungu. Mshahidi wa Yehova hukataa pia fundisho la kuwepo kwa utendaji wa Mungu katika nafsi tatu (3) za milele.
Ndugu msomaji wangu hiyo ndiyo imani ya dhehebu hili la mashahidi wa Yehova makala hii ya Tarumbeta ya Vitabu itaweka wazi na kutoa ufumbuzi juu ya mada hii ya msingi kupia vitabu mbalimbali vya dini hususani qur-an na Biblia Takatifu.
Jamii ya Waislam
Jamii ya waislam imejengwa chini ya msingi wa mafundisho na maelekezo ya Qur-an Tukufu, dini hii ya Uislam imeanzishwa rasmi mnamo mwaka 622BK mwaka ambao Muhammad alihama toka mji wa Makka kwenda Madina (Yathrib) akihofia mashambulizi aliyofanyiwa na Waarabu pamoja na Wayahudi mara tu alipotangaza kuanzisha Imani hii ya Kiislam.
Sehemu ya mafunuo ya Kiislam yaani Qur-an Tukufu huonekana kumtaja na kumwelezea Yesu kwa jina lile la Isa Ibn Mariam, lakini maandiko hayo humueleza Bwana Yesu (Isa Ibn Mariam) kama nabii tu na mtume wa Mungu kama walivyo mitume wengine.
Qur-an Surat Al-maida 5:75 Masihi bin Mariam si chochote ila ni mtume (tu). Bila shaka Mitume wengi wamepita kabla yake …………………..
Imani na maelezo hayo ndiyo yanayo chukuliwa zaidi na Ummah wa Kiislam na kutia mkazo zaidi kuwa Bwana Yesu yeye ni Mtume tu na hana cheo kingine au nafasi nyingine yeyote kimamlaka zaidi ya hiyo ya kiutume.
Pamoja na hayo jamii na Ummah huu wa kiislam unayochangamoto kubwa na mambo ya kutafakari kwa kina juu ya mamlaka haswa ya Bwana Yesu (Isa Ibn Mariam) hii ni kutokana na upande wa pili wa maelezo ndani ya Mafunuo na aya kadhaa za Qur-an ambazo huonekana kumfunua Yesu na kumpa heshma na mamlaka ya juu zaidi yanayoonekana kupita uwezo wa utendaji wa kiutume ama nabii tu. Maandiko hayo yatatusaidia sana kupitia jarida hili ili kupata ufumbuzi wa kina zaidi kuhusiana na asili na mamlaka haswa ya Bwana Yesu (Isa).
Jamii ya Kikristo
Jamii ya Wakristo (Manaswara ) wao pasipo hofu ukubaliana na vyeo pamoja na majina kadha wakadha aliyonayo Bwana Yesu kama aitwavyo.
-
Nabii - Yohana 4:19
-
Mfalme - Filipi 2:10
-
Mchungaji - Yohana 10:15
-
Njia - Yohana 14:6
-
Mwalimu - Marko 9:38
-
Bwana - Yohana 13:13 n.k.
Lakini pamoja na hayo huamini kuwa Bwana Yesu anayo mamlaka kuu zaidi ya hapo kiasili, yeye si mwanadamu wa kawaida tu. Pengine hilo tutalitazama mbele kidogo katika uchambuzi wa mada hii ili vitabu vyote vya Dini viweze kusaidiana na hatimaye kutupatia majibu sahihi na ya uhakika zaidi.
Hivyo Yesu aitwapo kwa majina hayo mbali mbali hulenga kuhashiria tu vile alivyo jishusha na kufukia kiwango na nafasi inayolingana na kumfikia mwanadamu (Emmanuel – God with us) ili kutekeleza mpango wa mbingu wa kumkomboa mwanadamu ambao lazima ufanywe na mamlaka kuu toka mbinguni lakini iliyojishusha.
Maelezo hayo yahusuyo imani ya wakristo juu ya bwana Yesu na mamlaka yake hukaziwa na waalimu wa Kikristo kupitia maneno ya Yesu mwenyewe anapotamka katika Maandiko:-