Sura ya Kwanza
Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu
------------------------------------------
Sura ya Pili
Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na Biblia.
---------------------------------
Sura ya Tatu
Je! Yesu ni nani haswa?
---------------------------------
Sura ya Nne
Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?
---------------------------------
Pr. Dominic Mapima
Muslim areas Evangelism Instructor.
Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com
WASIFU WA YESU KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA
Utume wa Paulo wathibitishwa
MZANI WA UTUME WA PAULO.
Mapitio ya mada:-
-
Historia ya Paulo dini na elimu.
-
Utume wa Paulo na uthibitisho wake.
-
Kukabili changamoto za upinzani wa utume wa Paulo.
-
Mwangaza wa utume wa Paulo katika Qur an na Biblia
1,Maelezo kuhusu dini ya Paulo
Kama ilivyo katika maandiko ya Biblia mtume Paulo haelezwi kama mtu aliyekuwa
katika misingi ya kipagani bali maandiko hayo hueleza wazi kuwa mtume Paulo
alikuwa ni mfuasi na mshika dini makini katika msingi wa dini ya kiyahudi huku akiwa
ni Farisayo aliyebobea.
Galatia 1:14 Nami naliendelea katika dini ya kiyahudi……………..
Matendo 26:4 Nalikuwa farisayo nikifuata dini na madhehebu yetu………..
Kile kilichokuwa ni kosa katika madhehebu hayo ya kiyahudi ni ile hali ya kung’ang’ana katika taratibu
na misingi ya sheria za kidini za mpito ambazo zilipaswa
kufikiliwa upya katika mtazamo wa Injili ya Kristo ambaye alikuwa tayari
amekwishakuja,hivyo kwa kuyashikilia mapokeo hayo ndiko kulipelekea mtume Paulo
na wakuu wake kuibua chuki dhidi ya wale walioikubali Injili ya Yesu na sera mpya
wokovu kwa kuhesabiwa haki kwa imani kupitia msalaba wa kristo.
Kumtazama matume Paulo katika jicho la Uislam
Kwa msomaji na mchimbaji mzuri wa elimu ya Uislam haitokuwa shida kwake
Kuelewa mtazamo huu wa historia ya Paulo au kuona wepesi wa kukubaliana
nayo kwakuwa historia kama hii inajirudia katika mwenendo wa dini ya kiislam
“ni nani katika Uislam asiyejua juu ya historia ya “Sayyidina Omary? Huyu alikuwa ni
Muuaji mkubwa wa watu wasiyo na hatia katika Saudi Arabia, lakini katika maisha
yake anaonekana kukutana na ujumbe wa Uislam na kuamua kusilimu ambapo
pia aliendelea katika dini ya kiislam kama askari mtetezi wa dini”.
“wakati wa kifo cha Muhammad ndiye aliyezuia watu kukubaliana na kifo hicho cha
mtume kwakuwa hakuamini kuwa mtume angaliweza kufa kabla ya kusilimisha dunia
nzima,alishika upanga mkononi akiwanyooshea waombolezaji waliokusanyika kwa
hasira kali na kutamka kuwa yeyote atakae sema kuwa mtume amekufa angemkata
kwa upanga huo.”Maisha ya Muhammad uk 79 – 82 by Shekhe Farsy.
Pamoja na historia hiyo ya wazi nilishangazwa na maneno niliyoyasikia katika
mihadhara wakati Fulani ambapo baadhi ya wahadhiri wa kiislam walionekana
kukanusaha juu ya utume huo wa Paulo kwa kigezo cha historia yake ya nyuma ya
uuaji ,pamoja nakuwa ilishapita baada ya kukutana na Yesu kama tutakavyoona hapo
mbele, hivyo mfano huu wa Sayyidina Omary ni ufumbuzi wa wazi wa hoja hiyo.
2. Utume wa Paulo na uthibitisho wake.
Historia ya utume wa Paulo katika msingi wa Biblia inaonekana kuanzia katika
Maelezo ya tukio la safari yake ya kikazi ya utekelezaji wa maagizo ya kuwatesa na
kuwabuluza kwenye magereza wale wote waliokubaliana na kweli ya Injili.
Matendo 9:1 kwa kadri ya andiko hilo tunaweza kuona ufupisho wa historia hiyo
yenye urefu kidogo kama ifuatavyo:-
-
Mtume Paulo akiitwa Sauli wakati huo alikuwa njiani kwenda Damesk kwa kusudi la utekelezaji wa hukumu kwa wakristo.
-
Akiwa njiani anaangazwa na nuru kutoka mbinguni.
-
Sauti ya malalamiko dhidi ya matendo ya Sauli inasikika ikisema mbona waniudhi?
-
Mtoa sauti hiyo anajitambulisha kuwa ni Yesu na hatimaye anamwelekeza kubadili mwelekeo na anachukuliwa kwenda kwa Anania.
-
Anania anasita kwa kuhofia matendo ya Sauli
-
Yesu anatoa tamko la kumchagua kama mjumbe wake mpya”Huyu ni chombo kiteule kwangu alichukue jina langu kwa mataifa”
-
Sauli abatizwa na kubadilishwa jina kuwa Paulo baadae kuanza kazi kama mtume wa kristo na kutangaza injili iliyombadilisha.
Ni imani yangu kuu kwamba mtililiko huo wa historia iliyoleta mabadiliko makubwa
kwa mtume Paulo na hatimaye kuteuliwa kwake kuwa mtume imekupa mwangaza
mpya wa imani toka katika mafundisho potofu yanayotolewa dhidi yake juu ya
uhalali wa utume wake.
Kutoka katika chanzo hicho mtume Paulo mwenyewe alijisikia ujasiri wa kuthibitisha
juu ya uhalali wa utume wake kupitia maelezo yake katika aya zifuatazo:
1Wakoritho 4:9 “Mungu ametutoa kuwa mitume wa mwisho.”
1Wakoritho 1:1 “Paulo aliitwa kwa mapenzi ya Mungu.”
Galatia 1:1 “Paulo si mtume wa wanadamu wala kuteuliwa na mwanadamu bali
Mungu na Yesu kristo.”
3.Kukabili changamoto juu ya utume wa Paulo.
Pamoja na uthibitisho huo wa utume wa Paulo kwa kadri ya ushahidi wa Biblia
tulikwisha uona, lakini bado hoja na maswali mengi yameendelea kuzalishwa na
kuulizwa na upande huo wa upinzani ambapo nimetolea majibu yake kama ifuatavyo:
a) Je, Paulo si mtume kwakuwa hayuko katika horodha ya mitume kumi na mbili?
Jibu:-
Kwa kadri ya Biblia tendo la Yesu kuchagua mitume kumi na mbili na kuwataja kwa
majina halikumaanisha kufunga uchaguzi au nyongeza ya mitume wengine, badala
yake tunaona jinsi alivyoendelea kuongeza kiwango cha idadi ya mitume ambao
wengine wao hata majina yao hayakutajwa katika mfumo au mtililiko maalumu katika Biblia.
Luka 10:1 “Kisha Bwana akaweka wengine sabini………”
Katika wazo hili huenda Paulo amepata fursa zaidi ya kiuthibitisho katika utume
wake kwa kadri ya mambo yafuatayo:-
-
aliyemtokea ni Yesu mwenyewe
-
alimtaja kwa jina
-
alimfanyia uchaguzi wa pekee
-
alitamkia wazi kuwa yeye ni chombo kiteule ili kulichukua jina la Bwana.
Jinsi hoja hii inavyohitimishwa na mafundisho ya Uislam na Qur an
Pamoja na kwamba hoja hii inakazwa na rafiki zetu wa upande wa kiislam lakini ni
jambo la kushangaza kuwa mafundisho ya Uislam yanaweza kutoa mwanga wa
majibu yake.
Fundisho la Uislam juu ya mitume/Manabii
Uislam unaamini na kufundisha juu ya kuwepo kwa wajumbe Manabii, Mitume zaidi
ya 124,000 (laki moja na ishirini na nne elfu).
Lakini hoja ya msingi ni kuwa pamoja na imani ya kuwepo kwa kiwango cha idadi
hiyo ya wajumbe hao bado maandiko ya Qur an yanataja jumla ya wajumbe 25 tu
katika aya kadhaa za kitabu hicho ambao ni:
Adam, Saleh, Lut, Hud, Yaakub, Ibrahim, Yunus, Musa, Daud, Al yaasa(Elisha),
Zakara, Dhul Kifli(Ezekiel), Isa, Nuh, Shuaib, Ismail, Yusuf, Is haq, Harun,
Suleiman, Yahya, Ayyub, Iliyas, Idrees, Muhammad.
Hao ndiyo mitume pekee wanaonekana kutajwa kwa majina katika mafunuo hayo
huku imani ya kiislam ikiamini juu ya kuwepo kwa zaidi ya mitume 124,000.
Katika hali hiyo Muhammad anaonekana kuelezwa yafuatayo katika mafunuo hayo ya
Qur an.
Qur an 40:78 Na kwayakini tuliwatuma mitume kabla yako, wengine katika hao
tumekusimulia,majina na habari zao na wengine hatukukusimulia
maelezo hayo ya Qur an yanaweka mkazo juu ya kuwepo kwa mitume wengine sahihi
ambao Muhammad hakuelezwa habari zao wala kutajiwa majina yao.
Kwa mtazamo huo wa Qur an binafsi ninapata changamoto ya msingi kwa rafiki zetu
wa kiislam kwa kuwaomba kujiuliza “kuwa wanapataje ushahidi wa kukanusha
utume sahihi wa Paulo na huku Qur an inaonyesha kutambua juu ya uwepo wa
mitume mbalimbali ambao hata wengine haikuwezekana kwa Muhammad
kutajiwa majina yao?
Je hakuna uwezokano wa kujikuta huenda tulikuwa tukikanusha matukufu ya
Mwenyezi Mungu pasina kujua kwa tendo la kuhukumu utume wa Paulo?
Endapo huu msomaji mzuri wa maandiko ya Qur an utagundua kuwa kamwe mafunuo
hayo hayamtaki muumini wa kiislam kuibua hoja au upinzani wowote pindi kuna
jambo linalo mtatiza bali muongozo ni huu:-
Qur an 16:43 waulizeni wenye kumbukumbu za vitabu vya Mwenyezi Mungu
vya kale ikiwa ninyi hamjui”
kwahakika endapo walimu na viongozi wa Ummah wa ndugu zetu wa kiislam
wangechukua hatua hii ya kimakusudi ya kurejea katika mafunuo ya Biblia katika
kutafuta ufumbuzi wa jambo hili wangeliweza kupata hakika na ufumbuzi wake
thibitifu hata hivyo bado hawajachaelewa.
b) Paulo anakanusha yeye mwenyewe kuwa si mtume
Hii ni hoja nyingine inayoonekana kutumiwa zaidi na wapinzani wa utume wa Paulo,
katika hoja hii wachambuzi wa vitabu wa kiislam wamekuwa wakinukuu maandiko ya
Biblia katika nyaraka za Paulo mtume na kuleta fundisho hilo.
1wakoritho 15:9 “Mimi ni mdogo katika mitume nisiyestahili kuitwa mtume maana
naliliudhi kanisa la Mungu.”
Katika andiko hilo kauli inayodhaniwa kuwa na utata ni pale mtume Paulo anposema
“mimi ni mdogo katika mitume nisiyestahili kuitwa mtume” maneno hayo bayana
ndiyo yanayofanya kuzuka kwa tafsiri na madai hayo ya kuwa hapo Paulo alikuwa
akikanusha kuwa yeye si mtume.
Jibu:-
Ni wazi kuwa watoaji wa tafsiri hiyo hawakuzingatia kanuni za kimsingi katika
taratibu za usomaji wa maandiko, moja wapo ya kanuni ya kimsingi ambayo
haikuzingatiwa ni ile ya kuelewa mfumo wa lugha na wazo la kihistoria katika kile
anachozungumzia msemaji au mwandishi.
Wazo la kihistoria katika kauli hiyo ya Paulo
Kimsingi maneno hayo ya Paulo yanaweza kuleweka vyema kwa kuzingatia wazo la
jumla la kihistoria ya maisha ya Paulo kabla ya kufikia hatua ya uteule wake wa kuwa
mtume wa kristo.
Kama nilivyokwisha dokeza mwanzoni mwa mada hii kuwa Paulo alikuwa ni farisayo
wa dini ya madhehebu ya kiyahudi waliokuwa ving’ang’anizi katika kutetea taratibu
na sheria za mpito za kidini na hivyo alikuwa mpinzani mkubwa wa Injili ya kristo na
mwuuaji wa wafuasi wa Kristo katika historia yake ya maisha ya nyuma.
Mfumo wa lugha alotumia Paulo
Kwa kurejea historia hiyo ya maisha ya nyuma ya Paulo na upinzani wake dhidi ya
haki ya Mungu unaweza kuelewa kirahisi zaidi kile mtume Paulo alichomaanisha
katika kauli yake hiyo”mimi ni mdogo katika mitume nisiyestahili kuitwa
mtume”.
Ni dhahiri kuwa alichomaanisha hapo si kukanusha utume wake halali bali ni kuonyesha kutokuwa na la kujivunia kwa kuteuliwa kwake huko kuwa mtume kwakua huenda asinge stahili fursa hiyo kwa kadri ya matendo yake ya awali.
“Paulo alitumia Lugha ya mwana mpotevu”
Lugha hiyo ya mtume Paulo inalingana bara bara na ile iliyowahi kutolewa na Mwana mpotevu kumbuka alisema “Sistahili tena kuitwa mwana wako” ni dhahiri kuwa kauli hiyo haiashirii kwamba yeye hakuwa mwana wa baba yule la” bali anaonyesha kushuka na kutokuwa na la kujivunia kwa rehema hiyo aliyotendewa licha kwamba alikuwa mkosaji.
Hata hivyo Paulo anasema Mimi ni mdogo katika mitume” hakusema Mimi si Mtume.
“Kauli ya Paulo katika kinywa cha Muhammad”
Kama ninavyo dumu kusisitiza wakati wote kuwa sehemu kubwa ya hoja na utata wa kidini ingewezwa kumalizwa kwa kulinganisha vitabu vyote vya kidini na kuona mfanano wa kauli na matukio.
Katika hili ni bayana kuwa ndani ya maandiko ya masaafu wa Qur an ziko kauli kadhaa zilizotolewa na Muhammad ambazo zinalingana kabisa na ile ya mtume Paulo, lakini kauli hizo kamwe hazikutafsiriwa na wanazuoni wa kiislam kama hatua ya Muhammad kukanusha utume wake:-
Hebu fuatilia aya hizi:-
Qur an 46:9 “Mimi si kiroja mpya katika mitume wala sijui nitakavyo fanywa mimi wala ninyi,
sifuati ila yaliyofunuliwa kwangu na sikuwa miye lolote ila ni mtu tu niliyefanywa
mtume.”
Qur an 7:188 “Sema sina mamlaka ya kujipa nafuu wala kujiondolea dhara ila apendavyo
MwenyeziMungu, na lau kama ningelijua ghaibu ningejizidishia mema mengi
wala lisingelinigusa dhara,mimi si chochote ila ni mwonyaji tu na mtoaji wa
habari njema kwa wanaoamini.”
Msomaji wangu hebu sasa chukua hatua ya kutafakari kwa uaminifu maandiko hayo ya Qur an,ni hakika yanatoa jumuisho la majibu na mwangaza wa ufahamu juu ya mada hii.
Kiukweli kauli hizo za Muhammad huenda pia zisingelifaa kulinganishwa na ile ya mtume Paulo kwakuwa huenda hizo ni za kujishusha zaidi kwa mfano jaribu kutafakari kauli hii” Mimi si chochote” au Sijui nitakachofanywa Mimi wala ninyi” na kisha jumuisha na ile ya awali “Mimi si kiloja mpya katika mitume.
Lakini kilichopo nikuwa hakuna kiongozi wa kiislam anayechukulia kauli hizo kama tendo la Muhammad kujiondolea sifa za kuitwa mtume bali badala yake kauli inayogeukiwa zaidi ni ile ya mtume Paulo katika Biblia nadhani ipo haja kwa wasomaji wa maandiko kulitafakari hilo upya tena katika mfumo huu linganifu.
Nini sababu nyingine ya Paulo kutoa kauli hiyo?
Pamoja na maelezo hayo ya uchambuzi nimeona pia iko haja ya kumuuliza mtume Paulo mwenyewe aweze kujieleza tabia yake katika mwenendo wake kwa Kristo itakayo tuwezesha kujua ujumla wa maana ya kauli yake hiyo. Hebu fuatilia aya hizi:-
2wakoritho 11:7 “Je nilifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe,
Kwasababu niliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?”
2wakoritho 10:1 “Basi mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa
Kristo, mimi niliye mnyenyekevu………”
2wakoritho 12:11 “Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa
nisifiwe na ninyi, kwasababu sikuwa duni ya mitume ya mitume
walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu.”
“Utume wa Paulo ni hakika kama unavyothibitishwa na maandiko ya Biblia”