top of page
Yaliyomo

Sura ya Kwanza

Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu

------------------------------------------

Sura ya Pili

Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na Biblia.

---------------------------------

Sura ya Tatu

Je! Yesu ni nani haswa?

---------------------------------

Sura ya Nne

Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?

---------------------------------

vlcsnap-2019-10-23-10h10m27s610.png

Pr. Dominic Mapima

Muslim areas Evangelism Instructor.

Mobile: 0754-527143

Email: dominicmapima@yahoo.com

Vitabu vya Chambuzi Mbalimbali
mosque.jpg

 WASIFU WA YESU KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA 

2.Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na Biblia.

Maelezo juu ya kuzaliwa kwa Yesu (Isa) yanaelezwa kwa upana zaidi kupitia maandiko ya vitabu vyote yaani ndani ya Qur-an katika sura ile ya 19 surat Mariam na kibiblia ni katika kitabu cha Injili ya Mtume luka 1:26 na kuendelea, hebu tuanze na mafunuo ya Qur-an tukufu vile yanavyoeleza kwa ujumla juu ya tukio hili la kihistoria.

 

Qur-an Surat Mariam 19:19 Malaika aksema hakika mimi ni mjumbe Wa Mola wako ili nikupe mwana Mtakatifu.

 

Qur-an hapa ina kubaliana na mawazo ya kimsingi juu ya tukio la malaika wa Mungu kupeleka ujumbe maalumu wa kuzaliwa kwa Yesu kwa binti huyu Mariam, katika aya za mbele ndani ya andiko hilo huonyesha tukio la Mariam kuhofia juu ya uwezekano wa kupata mtoto hadi anapo hakikishiwa juu ya nguvu na mkono wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe kushiriki na kuwezesha jambo hilo lisilo kubalika kibaolojia na kisayansi.

 

Mafunuo haya ya Qur-an hukamilisha tukio zima hadi kuzaliwa kwa masihi kuanzia aya ile ya 17 na kuendelea hadi 22 katika sura hiyohiyo  ya 19 (surat Mariam).

 

Mambo ya Kimsingi yanayoelezwa hapo.

Pamoja na tofauti ndogondogo tunazoweza kuziona lakini bado Qur-an hapo ufunua mambo ya kimsingi yahusikanayo na tukio la kuzaliwa kwa masihi Yesu (IsaIbn Mariam) kama ifuatavyo.

 

Yohana 8:23   Ninyi ni wachini mimi ni wajuu.  Ninyi ni wa

                       Ulimwengu huu mimi si  wa Ulimwengu huu.

​

  • Malaika alitumwa kupeleka taarifa rasmi ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu kwa Mariam

            (Aya 17)

  • Mariam alihofia juu ya kuwezekana kwa mpango huo ila  alifahamishwa kuwa uzazi  huo ni wa mkakati maalumu wa Mungu hivyo asihofu.

  • Uzazi wa Bwana  Yesu (Isa) ni wakimuujiza kwa Ulimwengu na niwa aina ya kipekee.        

 

Hayo ndiyo mawazo ya kimsingi juu ya uzazi wa Bwana Yesu yanayopatikana katika mafunuo hayo ya Qur-an, pamoja na hayo bado Qur-an itatusaidia kujua asili haswa ya Bwana Yesu (Isa) mbele kidogo ya mada hii muhimu naomba ufuatilie kwa makini.

 

Maelezo ya Kibiblia

 

Luka 1:26 mwezi wa sita malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mji wa Galilaya jina lake Nazaret, kwa mwanamwali bikira jina lake Mariam ………(2) utapata mimba na kuzaa mtoto mwanamume, naye ataitwa Yesu huyo atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa aliye juu.

   

Mtume wa Mwenyezi Mungu Luka Mtakatifu akiongozwa na roho mtakatifu (Ruh’ L-Qudus) anaweka wazi juu ya tukio hilo muhimu, ninayo imani kuwa Qur-an imepata habar kadha …….

kuhusu kuzaliwa kwa Bwana Yesu kupitia Mtume huyo Luka Mtakatifu kama Qur-an inavyojieleza yenyewe katika aya ifuatayo:-

 

Qur-an surat Al-Alaa 87:18 yaliyomo ndani  ya Qur-an yamo katika vitabu vilivyo tangulia, vitabu vya Musa, Isa na Manabii wengine.

   

Mtume Luka  anaweka wazi kuwa mamlaka ya Mbinguni ilimwagiza rasmi malaika mkuu Gabriel ili kuleta taarifa hiyo kwa Mariam juu ya kupata mimba na kumzaa mtoto ambaye anamtaja jina kuwa ni Yesu.

Pamoja na hayo aya za mbele zaidi huonyesha kuwa Bwana Yesu ataitwa mwana wa aliye juu, hapa pia huleta utata juu ya cheo na nafasi haswa ya Bwana Yesu, lakini kimsingi maandiko yanaonyesha kuwa jina hilo la mwana wa Mungu Bwana Yesu analipata baada ya tendo lake hilo la kuzaliwa na Mariam lakini bado ipo  asili haswa inayomhusu Yesu isiyotokana na vyeo au sifa alizopewa kutokana na kazi yake ya Utume wa Kidunia (Cross Culture witnessing)

 

Kumbuka            

Yesu alisema mimi ni wajuu ninyi ni wachini, Ninyi ni wa Ulimwengu    

huu mimi si wa Ulimwengu huu.

​

Qur-an itatusaidia kujua asili haswa ya Bwana Yesu (Isa) mbele kidogo ya mada hii muhimu naomba ufuatilie kwa makini.

 

Maelezo ya Kibiblia

 

Luka 1:26 mwezi wa sita malaika Gabriel alitumwa na Mungu kwenda mji wa Galilaya jina lake Nazaret, kwa mwanamwali bikira jina lake Mariam ………(2) utapata mimba na kuzaa mtoto mwanamume, naye ataitwa Yesu huyo atakuwa mkuu ataitwa Mwana wa aliye juu.

 

Qur-an surat Al-Alaa 87:18 yaliyomo ndani  ya Qur-an yamo katika vitabu vilivyo tangulia, vitabu vya Musa, Isa na Manabii wengine.

​

Je Yesu (Isa) ninani Kiasili?

 

Watu wengi wanaopenda kutafiti habari za Yesu wamekuwa  wakifanya kosa kubwa la kutotaka kujua asili ya Yesu kabla ya uzazi

 

wake wa kidunia, wengi wamekuwa wakifanya kosa hilo kubwa la kuhitimisha ufahamu wao juu ya Yesu kwa kuishia tu kumjadili mara baada ya kutwaa mwili pengine jambo hilo hutokana na kutokuwa na shauku ya kujifunza zaidi.

 

Lakini makala hii itatupatia mwanga. Maana tutavipa nafasi vitabu vyote viwili viweze kueleza Mamlaka haswa aliyokuwa nayo Yesu kabla ya kupewa majina ya Utume wake wa kidunia

 

Qur-an Tukufu inasemaje!

 

Qur-anSurat al-Imran 3:45 aliposema malaika ewe Mariam Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za “neno” litokalo kwake “jina lake” ni Masihi Isa Ibn Mariam, mwenye heshma katika Dunia na akhera ………….

 

Andiko hilo la Qur-an linaonyesha  na kufunua kwa wazi juu ya kauli ya Malaika kwa Mariam iliyomtaka kujua juu ya mamlaka inayotakiwa kukaa ndani ya tumbo lake na hapa Qur-an huitaja mamlaka hiyo kuwa ni Mwana aitwaye Isa Ibn Mariam. Lakini  Qur-an hutaja mwana huyo (Isa) kama “Neno” litokalo kwake (Mungu ). Katika maneno ya Kiarabu ni:“Kalimatu minhu”  - Neno litokalo kwake (Mungu)

 

Katika upana wa lugha neno “kalimatu” limetumika kama kisifa kinacho mwelezea “Mtu” maana imetumika kauli ya umoja, “Kalimatu”  - Neno, kwa Waarabu huita “Mufrada” yaani umoja hivyo aya haikusudii “Maneno” ya  kutamkika ila ni sifa na cheo cha mtu (Isa Ibn Mariam) kama Neno katika umoja na siyo wingi (Jami-u) hivyo Isa (Yesu) katika Qur-an hutambuliwa kuwa na cheo au sifa iitwayo Neno kabla ya zile za kibinadamu, katika Uislam manabii mbalimbali wamepewa …….

 

 

vyeo na sifa mfano:-

Musa huitwa   -           Takalama llahu………aliyeongea na Mungu

Ibrahimu        -           Habiba llahu ………    kipenzi cha Mungu

 

Lakini nabii  Isa huonekana kuwa na sifa mbili ya kwanza ni ile ya kuitwa

Kalimatu llahu                      -           Neno la Mungu

Ruh” llahu                             -           Roho itokayo kwa Mungu

 

Hivyo baada ya kufahamu hilo ni vyema sasa tukaangalia na kuchunguza kwa upana juu ya sifa hii ya “Neno” Je inatueleza nini juu ya asili na mamlaka haswaa ya Yesu  (Isa) kabla ya kuja hapa duniani.

 

Je Biblia inasema nini?

 

Baada ya kuona wazo hilo la Qur-an hebu tuone Biblia nayo inasema nini juu ya hilo?

 

Yohana 1:1-3  hapo Mwanzo kulikuwako neno  naye  neno alikuwa kwa Mungu, vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.

 

Katika sura na Aya hizo Biblia nayoinaeleza juu ya habari ya “Neno” (logos) pia inatupeleka mbele zaidi maana inasema kuwa huyo “Neno” (kalimatu) ni Mungu (rej …….Yohana 1: 1-2  naye neno alikuwa Mungu) Je hii inamaana kuwa huyo Neno ni Yesu! Na je inamaana Yesu ni Mungu kiasili?

 

Ndugu yangu mpendwa msomaji ukiwa ni Muislam au Mkristo yawezekana hilo likawa ndiyo swali lako. Ninakuomba kuwa makini zaidi tunapoingia sehemu hii ngumu na inayosumbua watu wengi.

 

Hebu kwanza tumfuatilie huyu Neno Je Biblia inasemaje juu ya Neno?

 

Zaburi    33:6     kwa “Neno” la Bwana Mbingu zilifanyika na Jeshi lake lote kwa

                          Pumzi ya kinywa chake.

​

Biblia hapo inaonyesha kutaja tena habari ya “Neno” na huyu neno hapo anaonekana kuwa na sifa ya kuumba, lakini ninayo imani  kuwa Biblia inapotaja habari ya “Neno” bado ingali inazungumzia juu ya Mungu mmoja tu katika upana wa utendaji (Nafsi) hivyo Neno ndiye Mungu huyo.

 

Je Neno la Mungu ndiye Mungu huyo?

 

Ndiyo ni kweli ndugu msomaji wangu hebu nikupe mfano:-

Kwa kutumia kielelezo cha Neno  lakawaida tunajifunza juu ya neno kama nafsi fikiri huenda ulimuudhi mtu Fulani naye kwa kughadhibika akaamua kukushitaki  kwa kosa la kumtamkia “Neno” baya  Swali! Je polisi watakapo kuja kukukamata watakamata “Neno” lako lililosema vibaya au utakamatwa wewe mwenyewe?

 

Jibu:-  Niwazi kuwa utakamatwa wewe mwenyewe na hiyo ni kwasababu! Neno na 

mwenye Neno  ni kitu kimoja.

Kielelezo hicho kinawiana fika na mamlaka ya Yesu kama Neno  la Mungu huwezi kumtenganisha kiasili na mamlaka ya Uungu, yeye (Yesu) ni Neno kama nafsi (logos) ya utendaji wa Mungu, alikuwako kabla ya vyote.

 

Pamoja na hayo ninaamini bado unajiuliza maswali haya.

Je! Huyu Yesu ninani haswa na je vitabu vyote vya dini vina uwazi gani kuhusu Yesu kama ni Mungu, na je kweli zipo dalili na sifa za Uungu wake?

 

Maswali hayo ni mazuri ikiwa yapo katika fikra zako ndugu msomaji wangu mpendwa.

 

Kumbuka  

Mungu ufahamika kwa vigezo na sifa maalumu zinazomfanya aitwa Mungu vigezo na tabia hizo kamwe havipaswi kumhusu mwanadamu. Vinginevyo ikiwa  yuko anayeonekana kuwa mwanadamu lakini vitabu halali vya Kidini yaani Qur-an na Biblia vikampa sifa za kimungu hiyo anapaswa kutazamwa  upya na kwa umakini, asije akawa ni Mungu pamoja nasi (Emmanuel).

 

Kumbuka

Mungu alijifunua kwenye kijiti na kusema na mtumishi wake nabii Musa (Qur-an 20:911)

Kulingana na ukuu na uweza wa Mungu huenda hilo lilikuwa ni jambo duni na lakushangaza ila Musa alipaswa tu kutambua kuwa alikutana na kuzungumza na Mungu na ndiyo sababu leo hii Musa huitwa katika Uislam.

 

Takalama llahu            -           aliyeongea na Mungu

 

Kubuka Musa alipoona ule moto alifikiri hata kuutumia kwa mambo binafsi lakini laajabu kumbe moto ule ulisitiri mamlaka ya Mungu aliye hitaji kuzungumza  naye.

 

​

​

bottom of page