top of page
Yaliyomo

Sura ya Kwanza

Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu

------------------------------------------

Sura ya Pili

Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na Biblia.

---------------------------------

Sura ya Tatu

Je! Yesu ni nani haswa?

---------------------------------

Sura ya Nne

Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?

---------------------------------

vlcsnap-2019-10-23-10h10m27s610.png

Pr. Dominic Mapima

Muslim areas Evangelism Instructor.

Mobile: 0754-527143

Email: dominicmapima@yahoo.com

Vitabu vya Chambuzi Mbalimbali
mosque.jpg

 WASIFU WA YESU KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA 

2. Siku ya Saba [Sabato] inavyoitwa katika Kiyunani,Kiarabu na Kiebrania

Ndugu mpendwa msomaji, neno hili Sabato hutumika katika misemo na lugha

mbalimbali za asili za kibiblia na hapa tunaweza kuona vile watu waliosema lugha kama Kiebrania na Kiyunani pamoja na Kiarabu walitamkaje neno hili Sabato, na lilileta maana gani:-

 

*     Waebrania huita         - Shabath

 

*     Wayunani huita          - Sabaton

 

*     Waarabu huita           -.Sabti

 

Matamshi haya yote pamoja na utofauti wake hutupatia maana moja tu nayo ni pumziko (rest) au kustarehe, na neno hili chanzo chake halisi ni mungu mwenyewe katika pumziko lake la siku ya saba ambayo hakufanya kazi yeyote (alistarehe - Sabato)

 

- Qur-an 7:54 –kisha akastarehe katika arshi .………….

- Mwanw 2: ]-4 - Bwana akastarehe siku ya saba.

 

Pamoja na hayo neno lenyewe Sabato huleta maana tu ya kustarehe [pumziko] hivyo ni rahisi tu mtu kujichagulia siku yake na kuiita Sabato, lakini jambo kuu ni kuwa bahati mbaya haitakuwa sawa na Sabato ile yenye maana ya siku ya saba katika siku za juma, ambayo mahasisi na mteuzi wake ni Allah (mwenyezi mungu) na siyo binadamu-

 

Kwa hakika mwanzo huo ndiyo utoa imani na ujasin kwa baadhi ya dini na

madhehebu kuweka siku zao za ibada, kwa kudai kuwa nazo huwcza kuwa Sabato tu - kumbuka mambo yafuatayo:-

 

a.    Sabato ya siku ya saba ilifunuliwa na kuhasisiwa na mungu mwenyewe kama Qur-an na Biblia visemavyo.

 

b.    Sabato ya siku ya saba imekazwa na kutiwa mhuri na Mungu mwenyewe

maana ndiye aliyeiandika kwa kidole chake mwenyewe kati ya amri kumi (Qur-an 7:'144 - 145. Kutoka 31:18)

 

c.    Sabato ya siku ya saba hutangaza ushindi wa Bwana katika ukomo wa

uumbaji na kuzaliwa kwa Dunia, kama kumbukumbu yako ya kuzaliwa.

bottom of page