top of page
Yaliyomo

Sura ya Kwanza

Mitazamo mbalimbali ya Kidini kuhusu Bwana Yesu

------------------------------------------

Sura ya Pili

Asili na kuzaliwa kwa Bwana Yesu (Issa) ndani ya Qur-an na Biblia.

---------------------------------

Sura ya Tatu

Je! Yesu ni nani haswa?

---------------------------------

Sura ya Nne

Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?

---------------------------------

vlcsnap-2019-10-23-10h10m27s610.png

Pr. Dominic Mapima

Muslim areas Evangelism Instructor.

Mobile: 0754-527143

Email: dominicmapima@yahoo.com

Vitabu vya Chambuzi Mbalimbali
mosque.jpg

 WASIFU WA YESU KWA MUJIBU WA QURAN NA BIBLIA 

1. Amri na hukumu katika maandiko ya Qur-an na Biblia

Jamii ya imani zote yaani Ukristo na ile ya Uislam, zinatambua kuwepo kwa Manabii na Mitume ambao Mungu aliwapa maono na mafunuo ya aina

mbalimbali ili kuwasaidia waja wa mungu.

 

Miongoni mwa manabii hao mmoja wapo ni Nabii Musa (alayhi salaam) ambaye katika imani ya Kiislam hutambuliwa kama Nabii aliyeongea na Mungu (Takalama llahu)

 

Mafunuo ya Qur-an yakiungana na yale ya awali ya Biblia huweka wazi mahali na jinsi nabii huyo alivyopata utume [unabii wake, katika kitabu cha Biblia habari hizo hupatikana katika kitabu cha Kutoka sura 3:1-10,

 

Maandiko hayo huungwa mkono na yale ya kitabu cha Qur-an tunaposoma

katika kitabu hicho katika sura ifuatayo:-

 

Surat Taha 20:3 "Nami nimekuchagua (kuwa mtume) basi yasikilize

                 unayoletewa (yanayofunuliwa kwako) wahyi."

 

Hapa Qur-an huonyesha tukio la kusimikwa kwa Nabii Musa na kupewa agizo la utame kwenda kwa Farao, [Firauni], hivyo hii inathibitisha vile ambavyo vitabu vyote hukubaliana juu ya utume wa nabii huyu [Musa alayh salaam],

 

Katika harakati za utume huo wa Nabii Musa ndipo tunaona akiwa katika safari ngumu ya kuwakomboa wana wa Israeli, na hatimaye baada ya kuvuka milima na mabonde anawafikisha chini ya Kilima kiitwacho Sinai.

Kama tujuavyo kibiblia kuwa hapo ndipo Musa alipo kabidhiwa mbao mbili za sheria na hukumu za Mwenyezi Mungu, ndivyo vivyo hivyo Qur-an pia huelezea kama tunavyo soma katika sura hii.

 

Qur-an Surat Al- A’raf 7:144-145

Akasema (Mwenyezi Mungu) "Ewe Musa mimi nimekuchagua juu ya watu wote kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu Basi pokea haya “niliyokupa" na uwe miongoni mwa wanaoshukuru.

 

[145] - Na tukamwandikia katiha mbao kila kitu mawudha (ya kila namna) na maelezo ya kila jamho "Basi yashike kwa imara bora haya, Karibu nitakuonyesheni miji ya wavunjao amri zetu ilivyoharibika na nitakuwalisheni ninyi.

 

Ndugu msomaji wangu. kama umefuatilia kwa uzuri aya hizo, yako mambo kadhaa ambayo utakuwa umeyagundua, binafsi nimeng'amua mambo yafuatayo:-

 

1.Kuna vitu ambavyo Musa aliitwa na kukabidhiwa na Mungu mwenyewe

(aya ya 144).

 

2. Vitu hivyo ni amri za Mungu, na aliye vikabidhi kwa Musa ni Mungu

Mwenyewe.

 

3. Aliye ziandika Amri hizo ni Mungu yeye mwenyewe (na tukamuandikia -

rejea aya ya 145)

 

4. Mungu hakuhitaji watu wazivunje amri hizo, ball wazishike kwa uhimara.

 

5. Mungu hakuwa na msamaha kwa wanao vunja amri zake tangu zamani.

 

Mpendwa msomaji kwa misingi hiyo, basi tunaona maandiko ya kitabu hiki cha msahafu wa Qur-an yanakubali tena kwa uwazi tu juu ya kuwapo kwa Amri za Mungu tena amri hizo hazikupaswa kuvunjwa, swali linalobakia ni kuwa, Amri hizo ni zipi? Naje Qur-an huzitaja amri hizo?

 

Katika utafiti wangu unaotokana na kusoma Qur-an mara kwa mara, nimeweza kugundua vile ambavyo Qur-an nayo hufunua amri hizo kumi ingawa si kwa maneno yanayo wiana sawa na yale ya Biblia bali wazo hubaki pale pale, kwa jinsi hiyo basi ninao ujasiri wa kueleza wazi kuwa Qur-an nayo huzitaja amri zote kumi kama ilivyo tangulia kukiri kuwa Mungu alikabidhi amri hizo kwa  Nabii Musa, na yeye mwenyewe ndiye aliyeziandika, hebu na tuone maarifa hayo mapya ndani ya Qur-an katika ulinganifu na yale ya awali ya Kibiblia.

 

Amri na hukumu katika Qur-an na Biblia.

          Biblia                                                                                     Qur-an

 

- Kutoka 20:1-3 usiwe na miungu Mingine        - Qur-an 17:22    usifanye miungu mingine

- Kutoka 20:4 usijifanyie sanamu ya kuchonga             - Qur-an 26:68-73 Je hizo sanamu

                                                                                                                       zitawasikia

- Kutoka 20:7   usilitaje bure jina la Bwana                 - Qur-an 7:180    usiharibu utukufu

                        Mungu wako                                                   wa majina ya mungu wako.

                  

- Kutoka 20:8   ikumbuke siku ya Sabato iutakase       - Qur-an 7:54     hakika mola wenu

                siku sita fanya kaziya saba ni sabato ya      mwenyezi mungu aliumba mbingu na

                 Bwana Mungu wako.                                   ardhi kwa siku sita kasha

                                                                                     akastarehe[siku ya saba]

                                

- Kutoka 20:12  waheshimu baba yako      - Qur-an 17:23    tuwaheshimu watu walio songa

                          na mama yako                                             [kuzidi] umri.

                       

- Kutoka 20:13  usiue                                      - Qur-an 4:29     msijiue wala msiue wenzenu

 

- Kutoka 20:14  usizini                                              - Qur-an 17:32    wala msiikaribie zinaa

 

-Kutoka 20:15   Usiibe                                   - Qur-an 17:35    pimeni kwa mizani iliyo sawa

 

- Kutoka 20:16  usimshuhudie jirani                         - Qur-an 22:30    mjiepushe na 

                          yako uongo                                                           usemi wa uongo

             

- Kutoka 20:17  usitamam mali ya mtu mwingne       - Qur-an 17:34    msitamani mali ya

                                                                                                               yatima.

Hivvo ndivyo tuonavyo Qur-an ikizitaja amr hizo katika aya tofauti na mfumo tofauti. kwa hiyo kwa msingi huo tunaweza sasa kufuatilia vyema mada yetu hii ihusuyo siku ya ibada ya Sabato katika mafunuo ya Qur-an.

 

Jambo Kuu

 

Kupitia uchambuzi huu wa amri kumi za Mungu- tumeweza kuona Qur-an ikiitaja siku ya saba yajuma na ya kuwa siku hiyo Mungu hakufanya kazi yeyote zaidi tu ya kustarehe- na hivyo Mungu alimjulisha Musa ill awahusie watu wake juu ya Jambo hili kama amri ya kuitambua siku hiyo. Ya mapumziko na kustarehe ambayo bila shaka ndiyo inayoitwa Sabato.

 

Ninaamini ndugu msomaji tumekwenda sambamba katika uchambuzi huu wa

mwanzo utakao tupa mwanga mkubwa wa kuelewa vyema maarifa haya juu ya

siku ya Ibada ya kweli, pamoja na hayo ninaamini kuwa huenda ukasumbuliwa sana hasa unaposikia neno Sabato- hivyo ili kukuandaa vyema ni vyema nikakupatia maana ya neno hili Sabato, nikihusisha na lugha mbali mbali za kigeni katika matamshi ya neno hili.

bottom of page