4.Ubinadamu wa Yesu, kwanini aitwe Mwana wa Mungu?
Ndugu mpendwa msomaji tutakubaliana kuwa hilo ni moja kati ya maswali nyeti yanayoulizwa na watu wengi wanao hoji na kutafiti mamlaka haswa ya Bwana Yesu.
“Ubinadamu wake”
Chanzo cha maswali yote yanayo ulizwa juu ya Bwana Yesu kinaanzia mara tu Yesu alipovaa mwili wa kibinadamu tendo hilo kwa fikra za haraka tu linaweza kudhaniwa kuwa ndilo linaloshusha mamlaka yake ya asili kama Mungu. Pamoja na hayo mimi binafsi nichoelewa ni kuwa tendo hilo kamwe halishushi mamlaka bali linafunika mamlaka aliyokuwa nayo kwa kadri ya sababu…………
Ifuatayo:-
Mungu aliwahi kujifunua wazi katika nyakati za nyuma na wanadamu wakaangamia
Fuatilia:- kutoka 19:14-19 “swali la kujiuliza”
Je! Mungu aje katika hali gain ili mwanadamu aweze kuikabili?
“Jibu”
Ni lazima uje katika hali inayofunika uwazi wa mamlaka yake iliyo ya utisho kwa mwanadamu mdhambi.
Fuatilia kutoka 33:18-20 mwanadamu hataniona akaishi ……………..
Sababu hiyo ya kimsingi ndiyo inayofanya Bwana Yesu kuchukua mwili wa kibinadamu kupitia Mariam kama tulivyo kwishaona. Hivyo mwili ya Bwana Yesu ulisitiri mamlaka kuu ya Uungu wake ambao hainge kuwa busara kuufunua na kufanya binadamu kuangamia badala ya kuokolewa naye. Kwa kauli nyingine ni kuwa Mungu (Yesu) alitumia mwili huo ili kuwafikia waja wake kama tulivyoona hapo nyuma jinsi Mungu alivyojifunua hata kwa kichaka kwa kadri ya Qur-an tukufu. “Ubinadamu ni njia ya Mungu kusema na waja wake:”
Qur-an 42:51 ……….. Mungu husema na wajawake kwa njia ya:-
-
Ilhamu – sauti ya ndani ya moyo ya Mungu
-
Nyuma ya pazia – ishara ya kufunika mamlaka.
Kwa kadri ya Aya hiyo tunaona Qur-an ikitaji “Pazia” kama chombo cha mawasiliana ya Mungu kwa wanadamu, pazia hii maanisha ni kitu kinachofunika ili kuzuia kuonekana kwa uhalisi wa jambo kwa lugha nyingine Mungu wakati Fulani huamua kufunika uhalisi wake kwa kujifunua nyuma ya “Pazia”.
“Pazia ni nini Kibiblia?”
Waebrania 10:20 ……….. ipitayo katika “Pazia” yaani mwili wake.
Katika Biblia Pazia huashiria mwili wa Bwana Yesu, hivyo hiyo ni njia ya kimawasiliano kati yake na binadamu inayofunika mamlaka yake ya Asili ya Uungu ili binadamu kumudu kukutana naye.
-
1Timotheo 3:16 Mungu alidhihirishwa katika mwili
-
Ebrania 10:5 Mwili uliniwekea tayari
-
Filipi 2:7 alijifanya hana utukufu …….. akawa na mfano wa mwanadamu.
Kwanini aitwe Mwana naye ni Mungu?
Tendo la Bwana Yesu kuitwa Mwana wa Mungu linaanzia kwenye chanzo cha kutwaa mwili.
Yohana 1:14 naye neno akafanyika mwili akakaa kwetu nasi tukaona utukufu wake utukufu
kama wa Mwana pekee atokae kwa baba …………..
Andiko hii linaonyesha hatua kuu mbili yaani:-
-
Kufanyika mwili
-
Kuitwa mwana atokae Mbinguni.
Sababu kuu
Tendo la Yesu kuamua kuchukua jukumu la kutuokoa lilimladhimu siyo kufunika Utukufu wake (Uungu ) tu kwa mwili bali pia kubadili kitambulisho chake cha mamlaka
“Fatilia mfano huu”
Maji yanaweza kugeuka katika hali mbalimbali katika kile ninachojua maji hayo mara yanapo badili hali tu pia tendo hilo huambatana na kubadilli jina, yaani mfano maji yanapoganda hanayoitwa tena maji bali huitwa barafu
Swali:- Je barafu si maji?
Jibu:- la barafu ni maji ila yamebadili asili kwa muda na baadae hurejea.
Sababu ya Bwana Yesu kuitwa mwana inatokana na kusudi lake tu la kuja Duniani Kutukomboa hivyo alifanyika barafu toka asili ya maji (alifaninyika mwana toka asili ya Uungu kama njia ya Ukombozi) lakini asili yake ya Uungu inabaki palepale.
Fuatilia ushauri mwingine juu ya Uungu wa bwana Yesu katika mafungu yafuatayo:-
Yohana 14:7-10……… aliyeniona mimi amemwona Baba
Tito 2:13 ……. Yesu Mungu mkuu na mwokozo wetu.
Yohana 20:28 Bwana wangu (Yesu) na Mungu wangu.
Ndugu mpendwa ninaamini hofu na mashaka ya moyo wako juu ya mada hii yamepingwa na uondolewa kupitia uchambuzi huu, fanya maamuzi yako leo kwa kujenga upya imani yako juu ya mamlaka ya Bwana Yesu kama tulivyo jifunza.
Hitimisho
Kwa mahitaji ya elimu na ufafanuzi wa mada mbalimbali zenye utata tafadhali niandikie au wasiliana nami kupitia anuani zangu kama nilivyoonyesha hapo chini. Masomo na vijarida mbalimbali vya huduma vimebariki watu wengi uwe mmoja wapo na Mungu atakujazi.
Lecture Prepared By Pr. Dominic Mapima
Muslim areas Evangelism Instructor.
Mobile: 0754-527143
Email: dominicmapima@yahoo.com