top of page
Vitabu vya Chambuzi Mbalimbali
mosque.jpg

4. Nini chimbuko la ibada ya siku ya ljumaa ya Kiislamu? Na Je, inasimama mahala pa Sabato?

Ulimwengu wa Imani ya Kiislam Duniani, unaadhimisha Ibada za mikutano mikuu katika siku ya ljumaa, ljumaa katika Uislam ndiyo siku inayodhaniwa haswa kuwa ni kivuli cha mahala pa Sabato (Jumamosi).

 

Pamoja na hayo ummah wa Kiislam kama isemavyo Qur-an, unatambua kuwepo kwa siku halisi ya ibada iitwayo Sabato (Jumamosi) isipokuwa, mafundisho ya viongozi wa Kiislam ndiyo huhafifisha nuru hii ya ukweli hasa ya siku ya Ibada (Jumamosi) na kukuza wazo hilo jipya la ibada ya siku ya ljumaa.

 

Viongozi na Maulamaa katika imani ya Kiislam, wamedai kuwa amri hii ya kiibada ihusuyo utunzaji wa Sabato halisi ya siku ya saba (Jumamosi), ilihusika haswa na kizazi cha Ban-israeli na yakuwa Mwenyezi Mungu alifanya mabadiliko mbele kwa kuwapa siku nyingine Ummah wa Mtume Muhammad.

 

Pamoja na maelezo hayo ya wanazuoni hao wa Kiislam, bado Qur-an inaonekana kuwa na msimamo wake endelevu juu ya wazo la taratibu ya amri za Mungu katika maagizo yake kwa wafata Dini. Hebu tuone nukuu ya aya hiyo:-

 

Qur-an 42:13 Amekupeni sheria ya Dini ile ile aliyomuhusia Nuhu

             na tuliyo kufunulia wewe na tuliyo wahusia Ibrahimu na

             Musa na Isa, kwamba simamisheni dini wala msifarikiane kwa

             hayo......................................................

 

Aya hiyo ya Qur-an inaweka wazi kuwa Mungu kamwe hawezi kubadili taratibu zake kwa sababu ya mabadiliko ya watu (Ummah).

 

Hivyo hata Muhammad alihusiwa juu ya sheria ya dini (njia) ile ile kama alivyo husiwa Ibrahim Musa na Isa, hivyo kamwe hapana kigezo chochote cha kimsingi kiletacho sababu ya mabadiliko katika mfumo wa Ibada kinachotokana na idhini ya Mungu mwenyewe.

 

Nini chimbuko la ibada ya siku ya ljumaa?

 

-     Ibada ya siku ya ljumaa huelezwa mwanzo wake katika kitabu kilicho andikwa na jumuiya ya vijana wa Ki Ansaar.

 

HISTORlA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) NA:- MUHAMMAD ABDALLA RIDAY ANSAAR MUSLIM YOUTH ORGANISATION UK. No. 47.

 

Hebu tuone maelezo mafupi katika ukurasa huo wa kitabu, katika kichwa Kisemacho.

 

IJUMAA YA KWANZA ALIYOSWALI MTUME.

 

Mtume aliondoka Qubaa kwenda Yathriba ilikuwa ni ljumaa, na jua lilipo chomoza alifika katika maskani ya Bani Salim bin Awf; katika Wangwa wa Ronunaa, hapo ndipo Muhammad aliposwali swala ya ljumaa kwa mara ya kwanza katika Uislam Na huo ni mwaka 622 uitwao mwaka wa Hijra kwa Waislam (mwanzo wa kalenda ya Kiislam).

 

Nini sababu ya Muhammad kusali siku hii na kuanzisha siku hii katika ummah wa kiislam?.

 

-     Mkazo mkubwa wa Ummah wa Kiislam juu ya siku ya ljumaa, unaanzia katika tukio hilo tu, maandiko ya Qur-an yanaonyesha wazi kuwa kabla ya hapo hata Muhammad mwenyewe alikuwa akifuata kawaida za ibada alizofundishwa na Wayahudi.

 

-     Wayahudi walikuwa na desturi ya kusali kwa kuangalia Yerusalemu, kawaida hii ndiyo iliyotawala maisha ya Muhammad kwa takriban zaidi ya mwaka mmoja na nusu naye alikuwa akiabudu kwa kuangalia Yerusalemu. (Qur-an 2:144 fafanuzi uk 34)

Tukio la mwaka 610 BK ndilo lililoleta mabadiliko makubwa kwa Muhammad, mwaka huo ndio ambao Muhammad alipokea mafunuo yake mapya katika mapango ya Jabal hilaa tofauti za kimafundisho, mwenendo, n.k zilianza kuonekana katika maisha ya Muhammad mara tu baada ya kuanza kupokea mafunuo hayo. (maisha ya Muhamadi uk 16 shekhe

Farsy).

 

-     Hilo lilimfanya Muhammad kuanza kupingwa na wayahudi hao, Haswa sababu kuu ni pale Muhammad alipoanza kupinga mafundisho waliyompa kama vile.

Kutia mkazo wa Kiibada katika jengo lenye asili ya upagani Al-Kaaba. Qur-an 22:29 [27:9] Qj

 

Kuanza kutangaza imani mpya ya uislam na kuwa na mafundisho yaliyo onekana kutofautiana na yake ya kibiblia.

 

-     Kutokana na mafunuo hayo mapya hoja kuu ya Wayahudi ilikuwa ni juu ya mashaka waliyonayo, kuwa mafunuo haya ya Muhammadi hayakuwa ya kweli, Aya ifuatayo ya Qur-an maonyesha hilo.

 

Qur-an Al-Baarah 2:97 Ufafanuzi uk 24 aya 97 hapa wayahudi

                      wanampinga Malaika Jibril amhaye ndiye aliyeleta

                      mafunuo hayo kwa Muhammad.

 

Ibada va liumaa inatokana na ugomvi wa Wayahudi na Muhammad.

 

-     Kutokana na hali hiyo mahusiano baina ya Muhammad na Wayahudi yaliharibika,

 

Fuatilia katika aya zifuatazo:-

 

Qur-an 5_:82 Maadui wa Uislam ni Wayahudi

Qur-an 2:I04 [Ufafanuzi] Wayuhudi walihitirafiana na Muhammad na kurushiana maneno.

 

Tangu hapo Muhammad hakupenda kamwe kuwiana na kile wanachofanya wayahudi katika mifumo ya kidini, na ndipo

anaitangaza rasmi siku ya ljumaa kama siku ya sala katika Ummah wa Kiislam wakati huo akiwa Yathrib (Madina),

 

-     Lakini pamoja na hayo Muhammad hakuipa siku hii nafasi ya Sabato yaani siku ya 7 ya juma (Jumamosi) ambayo ndiyo haswa iliyo siku ya Ibada ya kweli kama tulivyoona hapo awali,

 

-     Kumbuka siku ile ya kweli ya Ibada ilitengwa na Mungu yote iwe siku ya ibada tu na si kufanya kazi yeyote ya kimaisha. (Qur-an 7 : 163 Kutoka 20 : 8 )

 

-     Siku ya ljumaa haikutolewa ili kushika mahala pa Jumamosi [Sabato] maana pamoja na kufanya ibada Muhammad anaruhusu Waislam kufanya kazi siku hiyo mara baada ya swala, hebu tuone-

 

Qur-an 62:9-10 Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya sala

               siku ya ljumaa, enendeni upesi kumtaja Mwenyezi

               Mungu na acheni biashara kufanya hivi ni bora

               kwenu ikiwa mnajua basi fanyeni.

 

               [10] Na itakapokwisha sala, tawanyikeni katika

               ardhi mtafute fadhira za Mwenyezi Mungu.......

 

-     Ndugu mpendwa msomaji wa maarifa mapya hivyo ndivyo Muhammadi alivyoeleza juu ya siku hii ya ljumaa, kamwe siyo siku ya mapumziko kama ilivyo Sabato (Jumamosi) zaidi ya yote ljumaa si siku yenye mkazo wa kiibada kama ilivyo Sabato (Jumamosi). Katika mafunuo ya Qur-an.

 

-     Siku hii ya ljumaa ni siku ya ibada ya kawaida tu inayo ambatana na kufanya kazi za kutafuta kipato, hilo linaifanya kuwa na tofauti ya mbali sana na siku ya kweli ya Ibada ya Jumamosi.

 

Usifanye moyo wako kuwa mgumu,na usikimbie mahali pa raha yako, Sabato ya Jumamosi ndiyo siku halisi ya Ibada na siyo ljumaa "zinduka"

 

Je! Amri za Allah (Mungu) zinabadilika?

 

-     Msimamo wa wasomi wengi wa Kiislam katika jambo hili kuu, unaishia kwenye kudhani kuwa huenda kuna mabadiliko toka kwa Mungu mwenyewe juu ya Amri zake, na pengine Mwenyezi Mungu mwenyewe huadhimu kugawa sheria zake kwa makundi ya watu fulani maalumu tu na wenginekutotakiwa kuhusika nazo.

 

-     Wazo hilo si zuri ikiwa halitotumiwa kwa uangalifu, kimsingi tunachokizungumzia ndani ya kitabu hiki ni juu ya Amri za Mungu tena alizoziandika yeye mwenyewe, amri hizo ni amri za milele na vizazi vyote vya Dunia huhusika nazo na pia haziwezi kubadilishwa,

 

-     Ushahidi wa maandiko yafuatayo ya Qur-an utatupatia mwanga zaidi, kuwa je ni kweli kanuni hizo zinaweza kubadilika ati kwa sababu ya mabadiliko ya vizazi (Ummah)?

 

Qur-an Surat Ban Israel  17:77 Ndiyo desturi ya wale tuliowatuma

                              (tuliowapa utume) kabla yako katika

                               mitume wetu. Wala hutapata

                               mabadiliko katika desturi yetu.

 

Aya hiyo ya Qur-an inaweka wazi kuwa kamwe hakuna mabadiliko katika Kawaida ya Mungu aliyoifunua tangu mitume wa kale maneno haya yanaunga mkono kauli ya Bwana Yesu, pale aliposema sikuja kutengua Torati (Mathayo 5 : 17). bila shaka hata Mohammad hakustahili kuleta aina yeyote ile ya mabadiliko. pamoja na tofauti yake na Wayahudi. alipaswa kuzingatia tu kanuni za kimsingi za mafunuo ya Mungu mwenyewe kuhusu siku halisi ya Ibada (Jumamosi).

 

Qur-an Surat Fatir 35 : 43 wala hutapata mahadiliko katika kawaida

                           (desturi) ya Mungu (allyoiweka) wala

                           hutakuta mageuko katika kawaida  ya Mwenyezi

                           Mungu.

 

-     Kutokana na maandiko hayo ninapenda kukuhakikishia ndugu msomaji wangu kuwa ibada ya siku hii ya Sabato ingali inadumu kama ilivyo sehemu ya amri kumi ambazo kamwe hazibadiliki hata hivyo maandiko ya Qur-an yanaweka wazi kuwa Sabato ingali inadumu hadi mwisho kwa wale wanao mcha Miingu.

 

Qur-an Surat Al-Baqarah 2 : 66 kwa hivyo tukaifanya (adhabu hiyo)

                         kuwa onyo kwa wale waliokuwa

                         katika zama zao,na waliokuja nyuma

                         yao, na (tukaifanya) ni mawaidha

                         kwa wamchao Mwenyezi Mungu.

 

-     Aya hiyo inaonyesha adhabu waliyopewa watu waliovunja Sabato, na yakuwa walipewa adhabu hiyo ilikuwa onyo, kwa waliokuwa katika zama zao, waliokuja nyuma yao, na pia bado ni mawaidha (Mahusia) kwa watu wa zama hizi wanao mcha Mungu, Je wewe una mcha Mungu! Kama jibu ni ndiyo basi Sabato ni Ibada iliyo na nguvu kwako, anza kuitunza kwa kuabudu katika siku hii ya Bwana Mungu wako.

 

-     Ninakupatia wito huu wa pekee tafakari upya na ufanye maamuzi wakati ni sasa viongozi wa Dini, wazazi na marafiki hawatakuokoa tumtazame Allah, (laysa ila Lahu)

 

                                                                 *******TAMATI*******

bottom of page