Gundua
Miongozo Mbalimbali
MWONGOZO 1:
MWONGOZO 2:
MWONGOZO 3:
JE! MAISHA YANGU YANA MAANA KWA MUNGU?
MWONGOZO 4:
MPANGO KWA AJILI YA MAISHA YAKO
MWONGOZO 5:
DARAJA KWENDA KWENYE MAISHA YANAYORIDHISHA
MWONGOZO 6:
NAFASI YA PILI YA KATIKA MAISHA
MWONGOZO 7:
MWONGOZO 8:
MWONGOZO 9:
MWONGOZO 10:
JE! NI MAPEMA KIASI GANI YESU ATARUDI?
MWONGOZO 11:
UWEZO WA AJABU KATIKA MAISHA YANGUU
MWONGOZO 12:
MWONGOZO 13:
TOKA MDHAMBI MWENYE HATIA HADI MTAKATIFU ALIYESAMEHEWA
MWONGOZO 14:
MWONGOZO 15:
MWONGOZO 16:
MWONGOZO 17:
MWONGOZO 18:
SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA
MWONGOZO 19:
KUINGIA KATIKA MAISHA YA KIKRISTO
MWONGOZO 20:
MWONGOZO 21:
MWONGOZO 22:
MWONGOZO 23:
MWONGOZO 24:
MWONGOZO 25:
JE! NAWEZA KULIPATA KANISA LA MUNGU LEO?
MWONGOZO 26:
JE! MUNGU ANAO UJUMBE WA PEKEE KWA AJILI YA SIKU ZETU?
9. MAKAO YAKO YA MBINGUNI
Marko Polo aliporudi kwenye mji kusafiri miaka mingi katika nchi za mashariki, rafiki zake walidhani kwamba safari zake zile ndefu sana zilikuwa zimemfanya kuwa mwehu. Alikuwa na hadithi nyingi za kusimulia zilizokuwa hazisadikiki.
Marko alikuwa amesafiri hadi kwenye mji uliojaa fedha na dhahabu. Alikuwa ameyaona mawe meusi yaliyokuwa yakiungua moto, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amepata kuzisikia habari za makaa ya mawe. Aliiona nguo iliyokataa kuwaka moto hata kama ilitupwa katika ndimi za moto, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amepata habari za asbestos. Aliongea juu ya nyoka wakubwa urefu wao hatua kumi na mataya yao mapana ya kutosha kumeza mtu mzima, kokwa ambazo ukubwa wake ulikuwa kama kichwa cha mtu na nyeupe kama maziwa ndani yake [nazi], na kitu fulani kilichokuwa kikibubujika kutoka ardhini ambacho kilizifanya taa ziwake kabisa. Lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa amepata kuona, mamba, nazi, wala yale mafuta yasiyosafishwa.
Walicheka tu kusikia visa kama vile. Miaka mingi baadaye, Marko alipolala kitandani pake akiwa anakufa, mcha Mungu mmoja aliyekuwa kando ya kitanda chake akamsihi kuzikana zile hadithi zake ngumu za kusadadikika alizokuwa amezisimulia. Lakini Marko alikataa, alisema: "Zote ni za kweli kwa kila kipengele. Kusema kweli, mimi sijasimulia nusu ya yale niliyoyaona."
Waandishi wa Biblia watuonyeshao sisi picha kidogo tu ya mbinguni ambazo huonekana kana kwamba zinatoa mwangwi wa hisia aliyokuwa nayo Marko Polo. Katika maono yao walipatazama mahali pale palipokuwa paking'aa mno, pa ajabu mno, hata waliweza kueleza sehemu ndogo tu ya yale waliyoyaona. Nasi tunakabiliwa na changamoto ifananayo na ile ya marafiki wa Marko Polo. Hatuna budi kujaribu kuwaza habari za "mamba na nazi," yaani, mambo ambayo sisi hatujapata kamwe kuyaona kwa kuwa zile picha kidogo tu tunazozipata katika Biblia zinatuonyesha kwamba mbinguni ni zaidi ya kukaa juu ya mawingu na kupiga vinubi.
1. Je, Mbinguni Ni Mahali Halisi?
Yesu anatuandalia sisi mahali halisi kabisa hivi sasa katika mbingu iliyo ya halisi kabisa.
"Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi [Yesu]. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi kama sivyo, ningaliwaambia. Naenda KUWAANDALIA MAHALI. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, NITAKUJA TENA, niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo." - Yohana 14:1-3, KJV.
Yesu anakuja mara ya pili katika dunia yetu hii ili kutuchukua kwenda kwenye makao yaliyoandaliwa kukidhi utashi wa kila mtu katika mji wa mbinguni ulio na utukufu upitao ndoto zetu zote zilizochanganyikiwa mno; yaani, Yerusalemu mpya.
Baada ya kuishi kwa miaka elfu moja, Kristo anakusudia kuyaleta makao yetu ya mbinguni hapa katika sayari hii itwayo Dunia. Yerusalemu Mpya utakaposhuka hapa chini, moto utaitakasa dunia yote. Sayari yetu hii itakayofanywa kuwa mpya itakuwa makao ya kudumu ya waliookolewa. Ufunuo 20:7-15. mengi zaidi kuhusu suala hili yamo katika Mwongozo 22).
Je, Yohana, aliyekiandika kitabu cha Ufunuo, anatoa picha gani nyingine?
"Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule Mtakatifu, Yerusalemu Mpya ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi - arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi, ikisema, 'Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye ataisha pamoja nao. Watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao na kuwa Mungu wao" - (Ufunuo 21:1-3).
Baada ya nchi hii kubadilishwa kabisa kwa moto, je! ni akina nani watakaa katika ile nchi mpya?
"Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi" - (Mathayo 5:5, Angalia pia Ufunuo 21:7).
Kristo anaahidi kwamba dunia hii ambayo zamani ilikuwa kamilifu itarejeshwa katika uzuri wake ule wa Edeni, na wapole "watairithi nchi."
2. Je, Tutakuwa Na Miili Halisi Mbinguni?
Yesu alipowatokea wanafunzi wake akiwa na mwili wake uliofufuka na kutukuzwa, je, aliuelezaje mwili ule?
"Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa, kama mnavyoniona mimi kuwa nayo" - (Luka 24:39).
Yesu alikuwa na mwili halisi; alimtaka Tomaso amguse (Yohana 20:27). Wakati ule Yesu alitembea na kuingia katika nyumba halisi, na kuzungumza na watu halisi, na kula chakula halisi (Luka 24:43).
Kule mbinguni hakukaliwi na roho, bali na watu halisi wanaoyafurahia maisha ya kiroho, na ambao wana "mwili.. wa utukufu."
Nasi kwa hamu kubwa tunamngojea Mwokozi wetu kutoka kule, yaani, Bwana Yesu Kristo, ambaye, kwa uweza wake unaomfanya kuvidhibiti vitu vyote chini yake, ataibadilisha miili yetu hii minyonge ili ipate kufanana na mwili wake wa utukufu" - (Wafilipi 3:20,21).
Tunaweza kuwa na hakika kwamba miili yetu ya mbinguni itakuwa imara na ya kweli kweli kama ulivyokuwa mwili wa Kristo aliyefufukwa.
Je, tutaweza kuwatambua watu wa familia yetu pamoja na marafiki zetu kule mbinguni?
"Tuanachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapo baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi - (1 Wakorintho 13:12).
Kule mbinguni tutajua sana." Tutaelewana na kuthaminiana kwa kina kuliko tulivyopata kufanya katika dunia ya sasa.
Wanafunzi wa Yesu walimtambua akiwa katika mwili wake wa mbinguni, ni dhahiri kutokana na sura yake walipokuwa wamezoea kuiona (Luka 24:36-43). Mariamu alimjua pale kaburini kutokana na sauti yake aliyokuwa amezoea kuisikia wakati alipomwita kwa jina lake (Yohana 20:14-16). Emau walimtambua kutoka na ishara zake fulani za mikono walizokuwa wamezoea kuziona. Walipoangalia jinsi mgeni wao alivyokibariki kile chakula, walimtambua kuwa ni Bwana kwa tabia yake (Luka 24:13-35).
Waliokombolewa wanayo hakika ya kuwa na maisha ya kusisimua sana kwa kuungana uso-kwa-uso tena kule mbinguni. Fikiria furaha utakayokuwa nayo ukiitambua tabasamu ya aina yake ya mume au mke wako, au sauti inayokuita ambayo kwako inafahamika ya mtoto wako uliyemlaza kaburini zamani sana, ishara za mikono zinazoonyesha upendo kwako za rafiki yako fulani mpendwa wako. Tutakuwa na umilele utakaoimarisha vifungo vya maisha yetu kwa kina zaidi na kukuza urafiki wa karibu sana pamoja na watu wale wanaotuvutia sana katika ulimwengu.
3. Tutafanya Nini Kule Mbinguni?
Tutakuwa na shughuli nyingi za kutupatia changamoto kule mbinguni. Vipi kama wewe utaibuni mwenyewe nyumba yako unayoiwazia?
"Tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya… Nami nitafurahia Yerusalemu, na kuwaonea shangwe watu wangu… Watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mashamba ya mizabibu, na kula matunda yake… Wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi" - (Isaya 65:17-22).
Tayari Yesu anaandaa nyumba zetu binafsi katika ule Mji Mtakatifu, yaani, Yerusalemu Mpya (Yohana 14:1-3; Ufunuo 21). Mafungu hayo yanadokeza kwamba sisi pia tutabuni nakuzijenga nyumba nyingine - huenda zikawa ni zile nyumba zetu nzuri za mashambani, ambazo tutaziwekea mandhari nzuri sana ya mimea hai mbalimbali. Tena, basi, ni nani ajuaye ni mbinu gani za hali ya juu zinazotungojea kuzitumia katika ule ustaarabu wa juu zaidi wa Mungu? Uvumbuzi mpya wa sasa wa kisayansi, pamoja na safari ndefu zenye matukio mengi katika anga za juu zitaonekana kama mchezo wa kitoto tu tutakapoanza kufanya uvumbuzi wetu "nyumbani mwa Baba" yetu.
Je, unapenda uzuri wa maporomoko ya maji yanayounguruma, mashamba ya malisho matulivu, misitu mingi iletayo mvua, na maua mazuri yanayochanua?
"Maana BWANA ameufariji Sayuni;… amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika zake kama bustani ya BWANA; furaha na kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba" - (Isaya 51:3).
Mungu ataigeuza nchi hii itakuwa kama Bustani ya Edeni ya zamani. Hakuna tena kumwagika ovyo ovyo kwa mafuta, wala mchanganyiko wa ukungu na moshi, wala ukame; maziwa yatakuwa safi kama kioo, miti itakuwa na fahari yake, na mitelemko ya milima itakuwa bila waa lolote.
Sio tu uzuri wa dunia hii, bali pia uwezo wetu wa kuzingatia mambo utaongezeka sana. Utaonekana kama siku ya kwanza ya kutoka nje baada ya ugonjwa wa muda mrefu sana. Na zile "dakika ishirini za kuyaona mambo ya kweli" za awali zitaendelea na kuingia katika ule umilele wa kimiujiza.
Je, unafurahia kuyaona mambo mapya ? kujifunza? Kubuni vitu? "Kule, watu waishio milele watatafakari kwa furaha isiyokoma maajabu ya ubunifu wa uumbaji, siri ya upendo ukomboao… Kila uwezo wa kutenda kazi utakuzwa, kila uwezo wa kukumbuka au kujifunza utaongezeka. Kujipatia
maarifa hakutaichosha akili au kuzimaliza nguvu za mwili. Kule shughuli kubwa mno zitaweza kufanywa, hamu ya kuifikia hali bora kiroho itafikiwa, tamaa ya kufanya mambo makuu mno itatimizwa; na bado vilele vipya vya kuvipita vitainuka, maajabu mapya ya kuyastaajabia, kweli mpya za kuzifahamu, vitu vipya vitakavyohitaji kutumia nguvu za akili, roho na mwili. Hazina zote za ulimwengu zitawekwa peupe ili zipate kuchunguzwa na wale waliokombolewa wa Mungu." - Ellen G. White, The Great Controversy (Nampa, Idaho; Pacific Pres Publishing Asociation, 1950), ukurasa 677.
4. Je! Uovu Utaitishia Mbingu Tena?
"Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo" - (Ufunuo 21:27).
Mungu ataiondoa kabisa dhambi pamoja na athari zake za kutisha; mambo hayo hayataonekana tena. Yesu atakapoonekana, "tutafanana naye" (1 Yohana 3: 2). Badala ya kuipiga misukumo iliyo ndani yetu ya kuua, kuiba, kusema uongo, au kubaka, sisi tutaendelea kuwa na zile tabia nzuri za mbinguni.
"Naye [Mungu] atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakauwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita"- Ufunuo 21:4.
Hata yule adui yetu wa mwisho, yaani, mauti, atatoweka kabisa. Katika nchi ile ya mbinguni yenye ujana wa mielele wale waliokombolewa wanayo "miili isiyokufa" (1 Wakorintho 15:53); hakuna mwenyeji ye yote wa nchi ile atakayeteseka kutokana na uharibifu uletwao na uzee.
Sio tu kwamba hiyo mbingu inateketeza athari za dhambi, bali pia inafanya mageuzi ya athari hizo. Hebu fikiria itakavyokuwa kwa wale ambao wamepambana na ulemavu mbali mbali katika maisha yao yote:
"Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi
yatazibulia. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba" - (Isaya 35:5,6).
5. Je, Furaha Kuu Kuliko Zote Mbinguni Ni Ipi?
Hebu fikiria kwamba wewe unamwona Bwana wa malimwengu uso-kwa-uso.
"Tazama maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maisha yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, naye atakuwa Mungu wao" - (Ufunuo 21:3).
Mungu mwenyezi anaahidi kwamba atakuwa mwenzi na mkufunzi wetu. Ni furaha iliyoje hiyo kukaa miguuni pake! Hebu fikiria kile ambacho mwanamuziki angeweza kutoa ili kuweza kutumia dakika chache pamoja na Beethoven au Mozart. Fikiria jinsi mtaalamu wa fizikia ambavyo angeweza kuithamini sana nafasi ya kuweza kukaa chini pamoja na Albert Einstein, au ingekuwa na maana kubwa kwa kiasi gani kwa mchoraji kuweza kuongea na Michelangelo au Rembrandt.
Hebu fikiria tu jinsi wale waliokombolewa watakavyopata upendeleo mkubwa mno usio wa aina zote, sayansi yote, na sanaa yote. Watapatana kwa karibu sana na akili na moyo usio na kifani katika malimwengu yote. Na uhusiano huo utafurika na kugeuka kuwa ibada.
"'Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, 'asema BWANA" - (Isaya 66:23).
Katikati ya mji wa mbinguni kinasimama kiti kikuu cha enzi, cheupe, cha Mungu. Akiwa amezungukwa na duara ya upinde wa mvua wa zumaridi, uso wake unang'aa kama jua ambalo mng'aro wake unayatia macho kiwi. Chini ya miguu yake bahari ya kioo inakwenda pande zote. Katika sehemu ile ya juu inayong'aa kama kioo utukufu wa Mungu unaakisiwa [nuru yake inarudishwa], waliokombelewa wanakusanyika pale ili kutoa sifa zao kwa shangwe kuu.
"Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi,watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao, nao watapatwa na kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia" - (Isaya 35:10).
Hapa yupo mtu yule ambaye wema wake haukosi pigo hata moja. Uaminifu wake na subira yake na upendo wake huendelea tu milele zote. Na lihimidiwe jina lake takatifu!
6. Huna budi kuwa Kule!
Yesu anatamani sana kukutana nasi uso kwa uso wakati ule. Ndiyo maana yeye alipenda kukuokoa wewe kutoka katika dhambi kwa gharama kubwa kama ile. Wewe binafsi ni lazima unufaike kwa kuipokea zawadi hiyo. Ni lazima wewe ujitoe kabisa kwake Kristo awe Bwana na Mwokozi wako. Unahitaji msamaha wake unaotolewa kwako kutoka katika ule msalaba, kwa sababu:
"Ndani yake kamwe hakitaingia cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo ya uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo" - (Ufunuo 21:27).
Yesu anatuokoa kutoka katika dhambi [uvunjaji wa Amri Kumi], sio pamoja na dhambi [uvunjaji wa Amri Kumi]. Yatupasa kuja kwake kwa uwezo wake ulio ndani yetu na kutengwa mbali na uchafu na uovu. Yesu ni neno letu kuu la kuingilia katika ufalme wake unaokuja upesi.
Na ufalme ule unaweza kuanza sasa hivi ndani ya moyo wako. Kristo anapotuokoa sisi kutoka katika dhambi, anaiweka mbingu ndogo ndani ya moyo wetu. Anaweza kutusaidia sisi katika kushughulikia wasiwasi, hasira, tamaa ya mwili, hofu, na hatia inayotusumbua. Tumaini la kwenda mbinguni si njia ya kuyakwepa matatizo yanayotukabili katika maisha yetu; linasaidia kuileta mbingu kwa wingi zaidi hapa duniani. Kura iliyopigwa hivi karibuni ilionyesha kwamba "wale wanaoamini kwamba maisha yatakuwako baada ya kifo walikuwa na maisha yenye furaha na kuwa na imani na watu kuliko wale wasiosadiki hivyo."
Hakuna kitu cho chote kitakachokuwa na mvuto unaosisimua sana katika maisha yako ya wakati huu wa sasa kama kuwa na uhusiano wa imani na Yesu Kristo. Hebu sikiliza jinsi Petro anavyoeleza matokeo ya imani iliyo hai:
"Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka yenye utukufu, katika kumpokea mwisho wa imani yenu, yaani wokovu wa roho zenu" - (1 Petro 1:8,9).
Yote hayo utapata - pamoja na mbingu pia. Je! wewe umekwisha kugundua aina ile ya maisha tele ambayo Kristo anataka wewe uwe nayo? Tafadhali usigeuke na kwenda zako kwa kuukataa mwaliko wake huu wa neema.
"Na Roho na Bibi-arusi, wasema, 'Njoo!' Naye asikiaye na aseme, 'Njoo!' Naye mwenye kiu, na aje; na ye yote atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure" - (Ufunuo 22:17).
Yesu yu pamoja nawe hivi sasa, anazungumza na moyo wako unaposoma mistari hii. Anakualika wewe, anasema, "Njoo!" "Njoo!" "Njoo!" Asingeweza kuwa na shauku kubwa zaidi ya hiyo, asingesisitiza zaidi ya hivyo alivyokwisha kufanya. Kama wewe bado hujafanya hivyo, basi, hii ndiyo dakika yako ya kukichunguza kipawa chake hicho.
Kwa nini wewe usimwambie ya kwamba unakubali kukipokea kipawa chake hicho cha neema yake na ya kwamba wewe unataka kuishi milele pamoja naye? Mwambie kwamba wewe unampenda. Umshukuru kwa yote aliyokutendea na kwa yale ambayo unapanga kwa ajili yako. Kama kuna kitu cho chote kati yako na Mungu, basi, mwombe akufanye upende kuachana nacho. Leo hii, unapoisikia sauti yake, wakati moyo wako bado unavutwa kwake, jitoe kwake wewe mwenyewe bila kuacha kitu. Inamisha kichwa chako dakika hii na kusema, "Yesu, Bwana wangu, naja kwako. Nakupa wewe vyote nilivyo navyo. Mimi nataka kuwa wako milele hata milele.