Gundua
Miongozo Mbalimbali
MWONGOZO 1:
MWONGOZO 2:
MWONGOZO 3:
JE! MAISHA YANGU YANA MAANA KWA MUNGU?
MWONGOZO 4:
MPANGO KWA AJILI YA MAISHA YAKO
MWONGOZO 5:
DARAJA KWENDA KWENYE MAISHA YANAYORIDHISHA
MWONGOZO 6:
NAFASI YA PILI YA KATIKA MAISHA
MWONGOZO 7:
MWONGOZO 8:
MWONGOZO 9:
MWONGOZO 10:
JE! NI MAPEMA KIASI GANI YESU ATARUDI?
MWONGOZO 11:
UWEZO WA AJABU KATIKA MAISHA YANGUU
MWONGOZO 12:
MWONGOZO 13:
TOKA MDHAMBI MWENYE HATIA HADI MTAKATIFU ALIYESAMEHEWA
MWONGOZO 14:
MWONGOZO 15:
MWONGOZO 16:
MWONGOZO 17:
MWONGOZO 18:
SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA
MWONGOZO 19:
KUINGIA KATIKA MAISHA YA KIKRISTO
MWONGOZO 20:
MWONGOZO 21:
MWONGOZO 22:
MWONGOZO 23:
MWONGOZO 24:
MWONGOZO 25:
JE! NAWEZA KULIPATA KANISA LA MUNGU LEO?
MWONGOZO 26:
JE! MUNGU ANAO UJUMBE WA PEKEE KWA AJILI YA SIKU ZETU?
4. MPANGO KWA AJILI YA MAISHA YAKO
Baada ya mchungaji kuzungumza juu ya somo hili, "Kwa nini mimi namwamini Yesu," mwanaume mmoja kijana, aliyevalia vizuri, alimtembelea katika chumba chake cha kusomea na kusema naye kwa mshangao, "Hotuba yako usiku wa leo ilitoka katika Biblia yako. Hebu niambie, kama Yesu alipata kuishi hapa duniani, mbona historia haisemi habari zo zote juu yake?
"Hilo ni swali zuri," mchungaji akajibu alipogeuka na kuchukua vitabu kadhaa na kuviweka chini. "Lakini, kwa kweli, historia inasimulia habari za Yesu Kristo."
"Hizo ningependa kujionea mwenyewe," yule mwanaume kijana akajibu. "Vema, hapa ni barua ya 97 ya kitabu cha 10 cha barua za (Pliny) Ndogo, Balozi wa Roma katika nchi ya Bithinia, jimbo la Asia ndogo ya zamani. Plinio alimwandikia mfalme wa Dola ya Roma Trajani (Trajan), akimwambia habari za matukio katika jimbo lake. Tazama, hapa anaomba ushauri juu ya jinsi anavyopaswa kulishughulikia dhehebu jipya, yaani, Wakristo.
Anasimulia habari inayohusu kuongezeka kwao haraka sana na jinsi walivyoimba nyimbo za kumsifu Mungu zilizotungwa kwaajili ya kiongozi wao, yaani, Kristo. Pliny aliituma barua yake karibu na mwaka ule wa 110 B.K. Barua hiyo iliyoandikwa na Pliny inatoa ushahidi wa kihistoria wa yule mwanadamu, Kristo, na juu ya kuenezwa kwa imani yake katika siku zile za mitume wake."
Akiwa ameshangaa, mwanaume yule kijana alisema, "Hebu niambie zaidi!"
Mchungaji alipoendelea kukipekua kitabu kingine, aliongeza kusema hivi, "Mwanahistoria mwingine, aliyeishi kipindi kile kile kimoja na Pliny, alikuwa ni Tacitus. Katika habari zake za miaka zilizotengwa (Anals), kitabu cha 15, sura ya 44, anasimulia habari za uhasama aliokuwa nao Nero na mateso yake dhidi ya Wakristo wakati mji wa Roma ulipochomwa moto. Tacitus anaeleza kwamba neno hilo "Mkristo" linatokana na jina la 'Kristo.' Anataja kwamba Yesu Kristo, mwasisi wa dini ya Kikristo, alikuwa ameuawa na Pontio Pilato wakili wa Yudea, katika kipindi cha utawala wa mfalme wa Dola Tiberio. Maelezo haya yote anayotupa Tacitus yanalandana kabisa na matukio, majina na mahali palipotajwa katika Biblia."
"Mchungaji, mimi sikujua kabisa mambo hayo kuwa yalikuwamo katika historia ya ulimwengu.!" mgeni yule akasema kwa mshangao.
Mchungaji yule akaongeza kusema hivi, "Nataka uzingatie kwamba karibu na mwaka wa 180 B.K. Celsus aliandika kitabu akiwashambulia Wakristo, akionyesha kwamba kufikia wakati ule Ukristo ulikuwa ni nguvu iliyopaswa kutambuliwa.
"Kama wewe bado una mashaka, basi, kumbuka kwamba vitabu hivyo vinne vya Injili ni historia iliyosawa na ile ya vitabu hivyo vya kidunia."
Yule mwanaume kijana alipotambua kwamba historia zote mbili, yaani, ile takatifu na ile ya kidunia, zinakubaliana kwamba Yesu alipata kuishi hapa duniani kama mwanadamu, alikwenda zake akiwa ameamini kwamba Yesu Kristo alikuwa mtu halisi wa kihistoria.
1. Kristo Alikuwako Tangu Milele
Yesu hakuwa tu mtu mwema, alikuwa Mungu pia. Je, ni madai gani aliyoyatoa Yesu mwenyewe kuhusu Uungu wake?
"Kama mngalinijua mimi kweli kweli, mngalimjua na Baba. Tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.... Ye yote aliyeniona mimi amemwona Baba" - Yohana 14: 7-9.
Ukitaka kujua jibu kwa maswali haya, "Mungu ni nani? Anafananaje?" unapaswa kumtazama tu Yesu, aliyetangaza, akasema, "Mimi na Baba Tu umoja (Yohana 10:30.)
Mungu Baba na Yesu mwanawe wamekuokoa pamoja tangu milele (Waebrania 1:8.) Haukuwako wakati wo wote ule ambapo Kristo hakuwa umoja na baba yake. Baba yake anatoa upendo na ulinzi wake ule ule kwa kila mtu kama aliouonyesha Yesu katika kipindi cha maisha yake ya kibinadamu hapo duniani.
2. Kristo, Kiini Cha Historia Na Unabii
Kwa kuwa kisa cha maisha ya Kristo ni utimizo wa unabii, kisa cha maisha yake kiliandikwa kabla yeye hajazaliwa unabii wa Agano la kale huonyesha kwa kifupi kinachoeleweka wazi maisha yake, kifo chake na ufufuo wake kabla hayajatokea. Agano Jipya ni kisa cha maisha yake kilichoelezwa kama utimilizo wake. Wakiishi kuanzia miaka mia tano hadi elfu moja na mia tano kabla ya kuzaliwa kwake Kristo, manabii wale wa Agano la Kale waliotoa utabiri mwingi wa pekee kuhusu maisha yake Masihi, na tangu mwanzo kabisa wa kazi yake hapo duniani,
Watu walipoyalinganisha maisha yake na unabii wa Agano la Kale walifikia
hitimisho gani?
"Tumemuona yeye aliyeandikwa maisha katika torati na ambaye habari zake manabii pia waliziandika Yesu Nazareth Mwana wa Yusufu"_ (Yohana 1:45).
Mwokozi wetu aliwaelekeza watu kwenye unabii uliotimizwa ili kuthibitisha kwamba yeye ndiye:
"Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza yote yaliyosemwa juu yake katika Maandiko yote [ya Agano la Kale] kumhusu yeye mwenyewe" - (Luka 24:25-27).
Unabii uliotimizwa unatoa ushahidi unaosadikisha kwamba Yesu ndiye yule Masihi aliyeahidiwa.
3. Maisha Ya Kristo Ni Utimilizo Wa Unabii
Hebu na tuviangalie vifungu hivi vichache vya unabii huo toka katika Agano la Kale - na kutimizwa kwake katika kumbukumbu za Agano Jipya.
Mahali Pake Alipozaliwa
Unabii wa Agano la Kale: "Bali wewe BETHELEHEMU Efrata,.... kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli, ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele" (Mika 5:2).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Yesu alizaliwa BETHELEHEMU ya Yudea" - (Mathayo 2:1).
Kuzaliwa Kwake Na Bikira
Unabii wa Agano la Kale: "BIKIRA atachukua mimba, atazaa mwana, naye atamwita jina lake Imanueli [Mungu pamoja nasi]". - Isaya 7:14.
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu nyumbani kwako kama mkeo, maana MIMBA YAKE NI KWA UWEZA WA ROHO MTAKATIFU. Naye atazaa mwana, nawe utampa jina lake Yesu [BWANA huokoa]" - (Mathayo 1:20-23).
UKOO WAKE WATOKA KATIKA KABILA LA YUDA,... mpaka atakapokuja yeye anayeimiliki" - (Mwanzo 49:10).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Maana ni dhahiri kwamba BWANA WETU ALITOKA KATIKA YUDA" -(Waebrania 7:14).
Kukataliwa Kwake
Unabii wa Agano la Kale:
"Alidharauliwa na KUKATALIWA na watu" - (Isaya 53:3).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Alikuja kwa wale waliokuwa wake, lakini WALIO WAKE HAWAKUMPOKEA" - (Yohana 1:11).
Kusalitiwa Kwake Na Ujira Aliolipwa Msaliti Wake
Unabii wa Agano la Kale:
"MSIRI WANGU niliyemtumaini, aliyekula chakula changu, ameniinulia kisigino chake" - (Zaburi 41:9).
"Nikawaambia, "Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia
VIPANDE THELATHINI VYA FEDHA" - (Zakaria 11:12).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Wakati huo mmoja wa wale kumi na wawili, jina lake Yuda Iskariote - aliwaendea wakuu wa makuhani na kuwauliza, 'Ni nini mtakachonipa nikimsaliti kwenu? Wakamhesabia VIPANDE THELATHINI VYA FEDHA" - (Mathayo 26:14,15).
Kifo Chake Msalabani
Unabii wa Agano la Kale:
"WAMENIZUA MIKONO na miguu yangu" - (Zaburi 22:16).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Walipofika mahali paitwapo FUVU la kichwa, WAKAMSULIBISHA pale" - (Luka 23:33. Angalia pia Yohana 20:25).
Kutoka Kwake Kaburini
Unabii wa Agano la Kale:
"Maana hatukuachia kuzimu nafsi yangu, wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu" - Zaburi 16:10.
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
"Yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake HAKUACHWA KUZIMU, wala mwili wake haukuona uharibifu. Mungu amemfufua huyu Yesu, na sisis sote tu mashahidi wake" - (Matendo 2:31,32).
Ushahidi huo una nguvu kuonyesha kwamba Yesu hakutimiza utabiri mchache tu. Maandiko yahusuyo maisha yake kwa kweli yaliandikwa kabla yake kwa njia ipitayo uwezo wa kibinadamu. Kweli, Yesu ni Mwana wa Mungu.
Baada ya kuuangalia ushahidi huo, tunahitaji kufanya uamuzi wetu kwa njia ya maombi kuhusu nani atakayekuwa Bwana katika maisha yetu. Kama wewe bado hujafanya hivyo, je! utayaweka maisha yako mikononi mwake Yesu?
4. Maisha Yaliyopangwa Na Mungu
Yesu aliishi maisha yaliyopangwa na Mungu, ambayo yameelezwa kwa maelezo machache mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwake. Siku zote akiwa anautambua ukweli huo, alikuwa mwepesi kutambua maongozi ya Mungu. Kristo alisema:
"Sifanyi neno lo lote kwa nafsi yangu, ila nanena yale tu aliyonifundisha Baba... kwa sababu nafanya siku zote yale yampendezayo" - (Yohana 8:28,29).
Mungu alipanga maisha ya kibinadamu ya Yesu kabla ya kuzaliwa kwake, tena Mungu anao mpango kwa kila mwanadamu pia. Anajua jinsi kila mmoja wetu anavyoweza kutimiza haja zake zenye kina sana na kujipatia maisha tele.
Ray siku zote hakuwa na hakika kabisa iwapo alitaka kuufuata mpango wa Mungu. Lakini alipokabiliwa na uamuzi mkubwa kuhusu wapi alipaswa kwenda kusoma chuoni, basi, kwa mara yake ya kwanza katika maisha yake aliamua kutafuta uongozi wa Mungu katika suala lile. Aliomba kwa siku kadhaa na kujitahidi kusikiliza jibu la aina fulani. Baada ya muda fulani kupita alionekana amepata sababu zilizo wazi sana kwa nini angepaswa kuchagua chuo B: Chuo Kikuu kisicho na gharama kubwa sana, lakini kikubwa na ambacho hakiendeshwi na mtu fulani mahsusi. Mara tu baada ya kuanza kusoma pale alifahamiana na Wakristo fulani wa ajabu waliokuwa wamejiunga na chama fulani cha kumtetea Kristo katika eneo lile la kile chuo kikuu. Uzoefu wote aliokuwa nao pamoja nao katika kipindi cha miaka miwili iliyofuata uliyabadilisha maisha yake kabisa.
Ray anapoangalia nyuma leo, anaona kwamba kila wakati alipokuwa amekabiliwa na uamuzi mkubwa na kutafuta uongozi wa Mungu, "Mungu alinifunulia uwanja mpya wa maisha yangu."
Je, unawezaje kuujua mpango wa Mungu kwa maisha yako? Mungu anatoa uongozi wake kwa njia kadhaa:
i. Biblia
Kulingana na mtunga Zaburi, je! ni kitabu gani kinachoyaongoza maisha yetu?
"Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu" - (Zaburi 119:105).
Neno la Mungu huifanya upya mioyo yetu na kutupatia maarifa (Warumi 12:2, Zaburi 199:99). Wakati maalum uliopangwa kwa kujifunza Maandiko na kuomba ndiyo njia bora kuliko zote ya kuyaratibu mambo yenye kipaumbele.
ii. Maongozi Ya Mungu Katika Mambo Yanayotupata
Mungu anatuongoza pia kwa mambo yaongozwayo na Mungu mwenyewe. Zaburi 23 huonyesha yeye kama mchungaji mwema. Mchungaji
anawaongoza kondoo wake katika mabonde yenye majani mabichi sana na
kupitia katika makorongo yenye miamba. Anao uwezo wa kuwasaidia wale anaowapa maagizo yake ili wanufaike na kujifunza kutokana na kila jambo linalowapata katika maisha yao. Tunaye mchungaji anayeambatana nasi na kukaa karibu sana kando yetu.
iii. Mawasiliano Toka Kwa Mungu Ya Moja Kwa Moja hadi Moyoni
Mungu anatuongoza pia kwa njia ya kuzungumza nasi kupitia katika dhamiri zetu. Roho wake anaweza kuyatia nuru "macho ya mioyo yenu" (Waefeso
1:18). Kadiri tunavyozidi kufanya mazoezi ya kuwasiliana na Mungu ndivyo kadiri anavyoweza kutuongoza sisi. Anaziumba upya hisia zetu za ndani na uwezo wetu wa kufikiri na kuamua ili tupate kuiona wazi hatua inayaofuata ambayo tunahitaji kuichukua.
5. Maongozi Hayo Ni Lazima (Yapatane)?
Naam, yawezekana kudhani kwamba wewe unaishi maisha yanayoongozwa na Mungu wakati wewe unafuata tu mielekeo yako na hisia zako mwenye (Mithali 16:25). Hisia zetu ni lazima zipatane na mafundisho ya Biblia. Si salama kuamua kwamba ni Mungu anayetuongoza isipokuwa kama maongozi yote matatu yanapatana.
Hebu na tumchukue Jake, kwa mfano. Alikuwa na mke wake mzuri sana na watoto wawili, lakini alifanya uzinzi na mwanamke mwingine. Aliwaambia hivi rafiki zake: P "Mimi nimeliombea jambo hilo, nami najua kwamba hayo ni mapenzi ya Mungu."
Hisia za moyoni za Jake na "maono yake ya ndani" kwa dhahiri yalimpeleka katika njia ile mbaya iliyokwenda chini. Yeye aliwaza kwamba yale yalikuwa ni "maongozi ya Mungu"yaliyompelekea kukutana na mwanamke yule mwingine, wala hakurudi nyuma kuziangalia amri za Biblia dhidi ya uzinzi. Na Biblia hiyo, ambayo ni "sheria na ushuhuda," ndicho kitabu cha mwongozo chenye mamlaka, ndiye mwamuzi wa mwisho anayeamua njia sahihi ya kufuata katika utendaji wetu (Isaya 8:20). Kamwe tusiruhusu maoni yo yote au jambo lo lote linaloonekana wazi kuwa ni maongozi ya Mungu kutupeleka mbali na kanuni ya Biblia.
6. Kujikabidhi kwa Mpango Wa Mungu
Shetani alipokuja kumjaribu Yesu kule nyikani, alitoa shauri hili, "Kama wewe ukiachilia mbali kujitoa kwako mhanga kunakokuletea maumivu
makali, ambako Baba yako amekupangia wewe, mimi nitakupa dunia hii yote iwe mikononi mwako - pamoja na sifa, mali, na maisha ya raha mustarehe." Shetani akanukuu hata Maandiko katika jitihada yake ya kumfanya Yesu apotee. Lakini kila wakati Yesu alipambana naye na kumsukuma nyuma kwa maneno haya, "Imeandikwa" (Mathayo 4:1-11).
Fundisho moja lenye nguvu tuwezalo kujifunza kutokana na maisha yake Yesu ni utii wake kwa mapenzi ya Baba yake. Hata katikati ya maumivu makali ya kutisha ya Gethsemane, yeye akalia, kasema, "Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke. Walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe" (Mathayo 26:39). Baada ya ile miaka mitatu ya kazi yake, akiishi siku kwa siku kupatana na mpango wa Baba yake, Kristo alipokuwa akifa maneno yake yalikuwa ni haya: "Imekwisha" (Yohana 19:30). Yesu alikuwa akisema maneno haya hasa, "maisha yangu yaliyopangwa na Mungu sasa yamekamilika na kutimilika."
Unapoanza kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nawe kulingana na Neno lake, kupitia katika mambo yale yakupatayo yanayoongozwa na Mungu, na kupitia katika mawazo ya moja kwa moja, unaweza kujifunza kuyakubali maongozi yake hayo kwa moyo wako wote. Wewe pia waweza kuigundua furaha ya maisha yaliyopangwa na kuongozwa na Mungu.