top of page

Gundua

bible-study-lesson-tips-small-group-lead
Ugunguzi.jpg

Miongozo Mbalimbali

bible-png-clipart-12.png

MWONGOZO 1:

TWAWEZA KUMWAMINI MUNGU

​

MWONGOZO 2:

TWAWEZA KUIAMINI BIBLIA

​

MWONGOZO 3:

JE! MAISHA YANGU YANA MAANA KWA MUNGU?

​

MWONGOZO 4:

MPANGO KWA AJILI YA MAISHA YAKO

​

MWONGOZO 5:

DARAJA KWENDA KWENYE MAISHA YANAYORIDHISHA

​

MWONGOZO 6:

NAFASI YA PILI YA KATIKA MAISHA

​

MWONGOZO 7:

KUHUSU MAMBO YAKO YA BAADAYE

​

MWONGOZO 8:

YESU AJAPO KWA AJILI YAKO

​

MWONGOZO 9:

MAKAO YAKO YA MBINGUNI

​

MWONGOZO 10:

JE! NI MAPEMA KIASI GANI YESU ATARUDI?

​

MWONGOZO 11:

UWEZO WA AJABU KATIKA MAISHA YANGUU

​

MWONGOZO 12:

MWOKOZI ALIYEPO DAIMA

​

MWONGOZO 13:

TOKA MDHAMBI MWENYE HATIA HADI MTAKATIFU ALIYESAMEHEWA

​

MWONGOZO 14:

SIRI YA OMBI LINALOJIBIWA

​

MWONGOZO 15:

SIRI YA FURAHA

​

MWONGOZO 16:

SIRI YA PUMZIKO LA MBINGUNI

​

MWONGOZO 17:

SIRI YA UKUAJI KWA KUSHUHUDIA

​

MWONGOZO 18:

SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA

​

MWONGOZO 19:

KUINGIA KATIKA MAISHA YA KIKRISTO

​

MWONGOZO 20:

SIRI YA KUKUA KWA USHIRIKIANO

​

MWONGOZO 21:

JE! WENGI WANAWEZA KUKOSEA?

​

MWONGOZO 22:

JE! MUNGU ANA HAKI?

​

MWONGOZO 23:

JEHANAMU NI NINI NA IKO WAPI?

​

MWONGOZO 24:

MTU AKIFA, KUNA NINI BAADAYE?

​

MWONGOZO 25:

JE! NAWEZA KULIPATA KANISA LA MUNGU LEO?

​

MWONGOZO 26:

JE! MUNGU ANAO UJUMBE WA PEKEE KWA AJILI YA SIKU ZETU?

​

​

17. SIRI YA UKUAJI KWA KUSHUHUDIA

Larry alikuwa akifurahia maongozi yale mazuri, chai ya kijapani, wali mkavu, nyumbani kwa Bwana Komari wakati wageni wengine walipoanza kuzitoa Biblia zao. Wote wakamtazama na kumngojea. "Tafadhali tupe somo letu sasa?" Bwana Komari aliomba.

Larry alikuwa karibu amepaliwa na chai yake. Alikuwa amedhani kwamba mkutano ule wa dhifa (Karamu) ulikuwa wa kujifurahisha tu. Na sasa hakuweza kufikiri juu ya kitu chochote cha kusema.

​

Kwa kweli Larry alikuwa amefundisha madarasa mengi ya Biblia katika shule ya Kikrsito ya Lugha ya Kiingereza katika nchi ya Japan alikokuwa akifanya kazi. Lakini yalikuwa yameandaliwa vizuri. Aliweza kutoa maelezo juu ya Biblia kwa wepesi. Lakini kuweza kuzungumza habari za Mungu papo hapo bila kujiandaa vizuri… hilo lilikuwa ni jambo tofauti.

​

Larry alikuwa amezisikia hadithi zote za Biblia tangu utoto wake. Lakini hazikuwa na maana sana kwake kwa msingi wa kibinafsi. Alikuwa anafanya mambo aliyojua kwamba yalikuwa mabaya machoni pake Mungu. Angewezaje basi, kuwaambia wengine habari za Mungu ambaye yeye mwenyewe alikuwa hamjui kwa kweli?

Basi, akiwa ameketi pale kwenye kochi lile, amezungukwa na watu waliokuwa wakimngojea, mchezo wake wa viigizo bubu ulikuwa karibu kuporomoka. Katika saa ile ya hofu yake, fungu likapita kasi mawazoni mwake lililosema kwamba roho Mtakatifu aweza kutupa sisi maneno ya kusema tunapoletwa mbele ya watu kutoa ushuhuda wetu (Luka 12:12). Alitoa sala yake ya kufa na kupona kuomba msaada, kisha akaking'ang'ania kisa kile kinachojulikana sana ambacho aliweza kukifikiria: yaani, kisa cha mwana mpotevu.

Alipoeleza jinsi Mungu anavyowapenda sana hata wale ambao wanatangatanga mbali naye, Larry akajikuta anaongea moja kwa moja toka moyoni mwake. Maneno yake yalikuwa yakiwaingia wale watu. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake Larry alitambua jinsi Mungu alivyompenda sana.

​

Usiku ule Larry alipiga magoti kando ya Kitanda chake na kutoa maisha yake kwa Mungu ambaye hatimaye alikuwa ni wa kweli kwake. Kushuhudia juu ya upendo wa Mungu kulifanya jambo hilo kuwa zaidi ya jambo la kawaida la kuwazia tu. Sasa likawa ni jambo la kweli lililomshinda nguvu.

​

1. Yesu Anatupa Changamoto Ya Kukua Kwa Njia Ya Kushuhudia

Wanafunzi walikuwa wametumia miaka mitatu na nusu wakiyazingatia maneno na matendo yake Kristo, na hatimaye kifo na ufufuo wake. Yesu alipokuwa karibu kurudi mbinguni, aliwateua wanafunzi wake kuwa wawakilishi wake.

"MTAPOKEA NGUVU akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, NANYI MTAKUWA MASHAHIDI WANGU… hata mwisho wa nchi." Matendo 1:8. (Isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo, mafungu yote ya maandiko katika GUNDUA Miongozo yanatoka katika Toleo jimpya la Biblia la Habari Njema.)

​

Wafuasi wake Kristo waliitoa mioyo yao kwake bila kuacha kitu katika ile siku ya pentekoste, Kristo,yule aliyefufuliwa alikuwa ameyabadilisha maisha yao kwa uwezo wa Roho. Wakawa mashahidi, sio tu wa kufufuka kwake kimwii na kupaa kwake, bali pia wa uweza wake wa ufufuo uliokuwa umeyabadilisha maisha yao.

Sisi kama Wakristo tu mashahidi pia wa ufufuo wake Yesu katika maisha yetu wenyewe kwa kuwa tumeupokea uwezo wake utufanyao sisi kuwa wapya.

​

"Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja. Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja; kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote. Kila mmoja wetu amepewa neema kadri ya kipimo alichojaliwa na Kristo" - (Waefeso 2:4-7).

Tumehuishwa pamoja na Kristo, kwa hiyo, tunaweza ku"udhihirish(a) wingi wa neema yake." Naye anatutaka sisi tuzipeleke habari hizo njema kwa ulimwengu mzima kuhusu kile awezacho kufanya ndani ya maisha ya mwanadamu, kisha anatuahidi kwamba atakwenda pamoja nasi tukifanya hivyo (Mathayo 28:19-20).

​

H.M.S. Richards, muasisi wa huduma ya Redio ya Sauti ya Unabii, siku moja alitoa ushuhuda huu. "Mimi nimekwisha kuona badiliko ndani ya mioyo ya watu walioisikia hiyo injili ya Kristo. Nimesafiri kwenda katika nchi ambako jina la Mungu na la Kristo lililokuwa halijulikani kabisa mpaka kanisa lake lilipoipeleka injili kule. Nimewaona watu hao wakibadilika kutoka katika uchafu kwenda katika usafi, kutoka katika magonjwa kwenda katika afya, kutoka katika hofu ya daima ya mapepo na kuingia katika furaha ile itokanayo na kuishi maisha ya Kikristo. Nimekwisha kuona badiliko katika hadhi waliyonayo wanawake. Nimeziona nyumba za kweli za Kikristo zikijitokeza kutoka katika giza la kipagani. Katika kila nchi niliyotembelea nimeona maisha ya watu yakibadilika. Mimi najua kwamba injili yake Kristo… ni uweza wa Mungu uletao wokovu (Warumi 1:16). Najua kwamba kanisa linapoutangaza ujumbe huo wa injili, mabadiliko hutokea ndani ya mioyo ya wanadamu, nayo yanaonekana kwa macho katika maisha ya wale wanaoitikia mwito wake."

​

Mungu ametupa sisi wanadamu tulio dhaifu sehemu yetu maalum ya kufanya katika kazi hiyo inayosisimua sana kwa sababu kule kutoa ushuhuda wetu ni sehemu muhimu sana ya kukua kwetu. Ili imani yetu iendelee kuwa na afya, ni lazima itangazwe. Kama yule Larry alivyogundua kwa njia ya kuvutia sana, kugawa imani yetu kunatusaidia sisi kuwa nayo kwa utimilifu zaidi, na kutufanya sisi tukue.

​

2. Tunamshuhdua Kristo Kwa Namna Tuishivyo

Kijana mmoja mwanaume, aliyekulia katika nyumba iliyojaa matusi, siku moja alitoa maoni yake haya. "Niliwaangalia wazazi wangu ambao kwa kielelezo chao walinipa picha mbaya ya Mungu; sikuona kamwe kielelezo cha mtu yeyote mwenye ngozi juu ya mwili wake anayenipenda mimi." Watu wale wanaotuzunguka. Wanamhitaji sana mtu fulani atakayewapa picha nzuri ya Mungu. Wanamhitaji mtu fulani "mwenye ngozi juu ya mwili wake" ambaye atawaonyesha tabia nzuri ya dini. Kwa kawaida hubiri letu lenye nguvu nyingi kuliko yote mara nyingi ni namna sisi tunavyoishi. Kabla watu hawajayazingatia yale unayoyajua, ni lazima wajue kwamba wewe unawajali kwa kiasi gani. Petro anatusihi, anasema.

​

"MWE NA MWENENDO WENU kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ilihata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hiyo wamtukuze Mungu kila siku ya kuja kwake. HAYO NDIYO mliyoitiwa; maana Kristo mwenyewe aliteseka kwa ajili yenu, akawaachieni mfano, ili mfuate mwenendo wake" 1Petro 2:12,21.

​

Kwa kuwa "Kristo aliteswa" kwa ajili yetu pale Kalvari, basi, tunacho kielelezo cha upendo wake wa kujitoa mhanga ambacho ki karibu sana nasi. Upendo ule, ukijitokeza ndani yetu kama matendo ya upendo ambayo sisi tunawatendea wengine, unaweza kuwa uwezo wenye nguvu nyingi kiasi cha kuwavuta wasioamini kuja mikononi mwake Kristo.

​

3. Tunamshuhudia Kristo Kwa Njia Ile Tunayofikiri

Ibilisi alipomshambulia Yesu kule nyikani kwa vishawishi vyake vya kuamsha tamaa ya kula chakula, majivuno, na kiburi cha makusudi, Yesu alipigana naye na kushinda kwa kunukuu Maandiko (Mathayo 4:4,7,10). Kristo alikuwa amejiandaa kwa sababu alikuwa ameujaza moyo wake na zile kweli za Biblia. Humo ndimo vita hii inamoupata ushindi wake au kushindwa kwake-yaani, ndani ya mioyo yetu.

​

"Maana kama vile mtu afikirivyo moyoni mwake, ndivyo alivyo" (Mithali 23:7).

Wakristo wanaokua hufikiri mambo yale ya mbinugni. Wanaweka nguvu zao zote katika kujenga tabia zile nzuri wanazojitahidi kuwa nazo.

"Furahini katika Bwana siku zote,… katika kila neno kwa KUOMBA na kutoa dua zenu, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, ITAWAHIFADHI MIOYO YENU NA NIA ZENU katika Kristo Yesu. Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya KWELI, yoyote yaliyo ya STAHA, yoyote yaliyo ya HAKI, yoyote yaliyo SAFI, yoyote yenye KUPENDEZA, yoyote yenye SIFA NJEMA - iwapo kitu chochote ni KIZURI SANA ua KINA SIFA NZURI- yatafakarini mambo kama hayo…. Na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi. "- (Wafilipi 4:4-9).

Kile tunachoilisha mioyo yetu kinaleta tofauti kubwa sana. Ukiweka uchafu ndani yako, utatoa nje uchafu. Ukiweka Neno la Mungu ndani yako, utatoa nje maisha yake Mungu.

​

4. Tunamshuhudia Kristo Kwa Namna Sisi Tunavyoonekana

Akiwa mwakilishi wa Kristo, Mkristo atakuwa na adabu hata kwa namna anavyoonekana kwa nje, akiepuka kuzidi kiasi kwa njia yoyote ile.

"Inanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako waume wo wote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno, kwani wataona jinsi mwenendo wenu ulivyo safi na wa kumcha Mungu. Katika kujipamba kwenu msitegemee mambo ya nje nje, kama vile mitindo ya kusuka nywele, kujivalia vitu vya dhahabu na nguo maridadi. Bali uzuri wenu unapaswa kutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wema na utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwaa mbele za Mungu. Ndivyo walivyojipamba hapo kale wanawake waadilifu waliomtumainia Mungu; walijiweka chini ya mamlaka ya waume zao"- (1Petro 3:1-5).

​

Kuvaa mavazi na mapambo ya kawaida kumedhihirisha daima uzuri ule wa kufanana naKristo. Kwa mfano ulio mkamilifu, wengine wangeweza kuvutwa kuja kwetu kwa kuwa sisi tu Wakristo, sio kwa sababu ya maneno yetu tunayosema juu ya mitindo ya kisasa, bali kwa maneno ambayo maisha yetu yanamtangaza Yesu.

​

5. Tunamshuhudia Kristo Kwa Namna Tutendavyo

Mwanahistoria Edward Gibbon anatuambia sisi kwamba Galerio (Galerius) alipoliteka kambi la Waajemi, mfuko wa ngozi unaong'aa uliojazwa lulu uliangukia mikononi mwa askari mmoja aliyekuwa akiteka nyara. Mtu yule aliutunza kwa uangalifu sana mfuko ule wenye manufaa, lakini lulu zile za thamani akazitupilia mbali.

​

Watu wale wanaozing'ang'ania furaha za juu juu tu ambazo ulimwengu huu unaweza kuwapa - huku wakimtupa Yesu mbali, Lulu ya Thamani kuu - wako katika hali mbaya sana kuliko yule askari aliyeteka nyara zile. Si mali tu iwezayo kuteleza mikononi mwetu, bali na uzima wa milele. Kwa hiyo Maandiko yanatuonya, yanasema:

"Msiipende ulimwengu, wala cho chote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwa ndani yake. Vitu vyote vya ulimwengu - tamaa mbya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali - vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu. Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele" - (1 Yohana 2:15-17).

​

Shetani anafanya kazi yake kwa bidii nyingi sana kupaka dhahabu nje ya dhambi zile zinazoangamiza watu sana na yale mazoea mabaya kabisa. Matangazo ya vileo huwaonyesha tu watu wale ambao ni vijana, wazuri, wachapa kazi, na wenye furaha nyingi sana. Hatumwoni mtu ye yote anayetoka katika duka la vileo akichechemea kama kinyago na kuwa na kisalfeti (gunia) mkononi mwake.

​

Tunapaswa kuwa waangalifu kuhusu marafiki wale tunaoshirikiana nao ili tusije tukaziacha kanuni zile za Kikrsito (2 Wakorintho 6:14). Kwa kweli, Kristo anatutaka sisi kuendelea kuwatembelea marafiki zetu hao wasiokuwa Wakristo. Uhusiano wetu na mtu mmoja mmoja ndizo njia za msingi ambazo kwanza imani yetu inagawanywa kwa wengine hakikisha tu kwamba rafiki zako hao hawakuvuti kukurudisha katika mwenendo wako ule wa zamani.

​

Kile tunachokiingiza katika maisha yetu, hata burudani tunayoichagua, vinalo shinikizo lake juu ya maisha yetu ya Kikristo. Tunahitaji kukitambua kile tunachoilisha mioyo yetu.

"Sitaweka mbele yangu neno la uovu" - (Zaburi 101:3).

Tukiilisha mioyo yetu kile kilicho bora kabisa, basi, kile kilicho kiovu kabisa hakitaweza kutuvutia chini ili tupate kufanana nacho. Kule kuzishikilia sana zile kanuni za juu zaidi katika vitu vile tuviletavyo nyumbani na mioyoni mwetu hakutayafanya maisha yetu kubanwa sana. Mkristo anayo mengi ya kumfanya awe na furaha kuliko mtu mwingine awaye yote.
("Wanionyesha njia ya kufikia uhai; kuwako kwako kunijaza furaha kamili, katika mkono wako wa nguvu mna mema ya milele") ( Zaburi 16:11).

​

6. Tunamshuhudia Kristo Kwa Utoaji Wetu

Alipokuwa karibu kumbatiza muumini mmoja mpya, hayati Mchungaji H.M.S. Richards aligundua kwamba yule mtu alikuwa na pochi ya fedha iliyokuwa imjeaa vizuri katika mfuko wake. Richards akamwuliza endapo alikuwa amesahau kuiacha fedha yake ile katika chumba cha kubadilishia nguo. "Mfuko wangu huu na mimi tutabatizwa pamoja," alieleza yule mtu. Alikuwa ameipata roho halisi ya Ukristo - yaani, kutoa ili kuwasaidia wengine. Wakristo hukua kwa kutoa na ndiyo maana "Yesu mwenyewe alisema. "Ni heri kutoa kuliko kupokea". (Matendo 20:35). Kile tutoacho ili kuendeleza ufalme wa Mungu kinaendelea kuwa na thamani ya milele.

​

"Msijiwekee hazina zenu duniani, nondo na kutu viharibupo, na wezi huvunja na kuiba. Bali JIWEKEENI HAZINA ZENU MBINGUNI. Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako"- (Mathayo 6:19-21).

Unapotoa kumbuka" Dunia ni mali ya BWANA, na vyote viijazavyo" (Zaburi 24:1), hii ni pamoja na fedha na dhahabu (Hagai 2:8). Sisi wenyewe tu mali ya Mungu,. Kwa sababu alituumba na kwa sababu yeye alituokoa kutoka katika dhambi zetu kwa kulipa fidia ya dhambi zetu kwa damu yake (1Wakorintho 6:19-20). Kila kitu tulicho nacho ni mali ya Mungu, kwa sababu yeye ndiye "a(tu)paye nguvu za kupata utajri" (Kumbukumbu la Torati 8:18).

​

Ni kiasi gani anachotaka tutoe, huyo Bwana wetu aliyesulibiwa na kufufuka, ili tupate kushirikiana naye katika kuipeleka injili kwa wengine?
"Je! mwanadamu atampora Mungu? Lakini ninyi mnanipora mimi. Lakini ninyi mwasema, "Tumekupora kwa namna gani?
"Mmenipora ZAKA NA SADAKA…
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu. Mnijaribu kwa njia hiyo,' asema BWANA wa majeshi; Mwone kama SITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI na kuwamwagieni baraka hata hamtaweza kuwa na nafasi ya kutosha kuiweka hiyo baraka" - Malaki 3:8-10.

​

Zaka ni "Sehemu ya kumi" ya mazidio" yote (Kumbukumbu la Torati 14:22, KJV; Mwanzo 28:22). Kwa mkulima au mfanyabiashara mazidio hayo ni mapato baada ya kutoa gharama za biashara (mtaji). Kwa mfanyakazi, ni mshahara wake kamili. Kanuni ya kutoa zaka ni kanuni ya kimaadili kwa sababu inahusu tabia ya mtu. Tunaposhindwa kutoa zaka huwa tuna "mwibia" Mungu. Zaka ni ya Mungu, nayo inatakiwa kutumika kwa ajili ya kuwapa riziki yao wachungaji wake Kristo peke yao (1Wkorintho 9:14), na kuimaliza kazi yake duniani ili yeye apate kurudi (Mathayo 24:14).

Yesu alipokuja hapa kuishi kati yetu, alitoa idhini yake ya kulipa zaka katika nyakati za Agano Jipya (Mathayo 23:23).

​

Je! hivi tutoe kiasi gani kama sadaka? Sadaka ni mtu mwenyewe anavyoamua kutoa. Kila mtu anatakiwa "atoe kama alivyokusudia kutoa moyoni mwake" (2Wakorintho 9:5-7). Wewehuwezi kumpita Mungu katika utoaji.

"Toeni, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa, na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndivyo mtapewa mapajani mwenu" - (Luka 6:38).

H.M.S. Richards siku moja alisimulia kisa hiki.

"Mpiga kamari mmoja aliyebobea katika maisha yake yote alihudhuria mikutano yangu kule Los Angeles, wala sitasahu kamwe wakati ule nilipozungumza naye tukiwa peke yetu nyuma ya ukumbi wa mikutano. Alitoa bunda la noti mfukoni mwake, Dola za Kimarekani 500, na kunipa mimi zote, huku akisema, "Hii ndiyo zaka yangu ya kwanza.!
"Yule mtu hakuwa mzima, naye alikuwa hajafanya kazi nyingine yoyote isipokuwa kupiga kamari kwa miaka 30 au 40 hivi, basi mimi nikamwuliza, utaishije kuanzia sasa?
"Alijibu, Nimebakiwa na dola tano au sita hivi, lakini hizo nyingine ni mali ya Bwana. "Kisha nikamwuliza, utafanya kazi gani, basi?
"Sijui, alijibu, ila najua kwamba ni lazima nitoe zaka yangu kwa Mungu, yeye atanitunza.!
"Na kwa hakika Mungu alimtunza. Toba ya mtu yule ilikuwa ya kweli. Alikwenda njia yote katika kujitoa wakfu kwake, naye alikuwa na furaha katika maisha yake ya Kikristo. Na Mungu hatoi ahadi kwamba waumini wote waaminifu watakuwa matajiri. Lakini tunayo ahadi kwamba Muumabaji wetu atatupatia mahitaji yetu ya maisha.

​

Kristo alitoa kila kitu kwa ajili yetu. Hebu sasa na tumpe kabisa mioyo yetu. Hebu na tuwaambie wengine habari zake Kristo kwa namna sisi tuishivyo, tufikirivyo, tuonekanavyo kwa nje, tutendavyo, na tutoavyo. Kwa nini sisi tusiigundue furaha hii ya kuwaambia wengine habari za Kristo na kuendelea kukua katika neema yake ya ajabu?

 

​

​

​

​

bottom of page